Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wayne Rooney amtupia zigo la lawama Wirtz

Rooney Pict
Rooney Pict

Muktasari:

  • Staa huyu ambaye anakutana na wakati mgumu tangu ajiunge na Liverpool akitokea Bayer Leverkusen dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa Pauni 116 milioni, msimu huu amecheza mechi nane za michuano yote.

LIVERPOOL, ENGLAND: LEJENDI wa Manchester United, Wayne Rooney amemtaja staa wa Liverpool, Florian Wirtz ndio anaharibu mfumo wa kocha Arne Slot.

Staa huyu ambaye anakutana na wakati mgumu tangu ajiunge na Liverpool akitokea Bayer Leverkusen dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa Pauni 116 milioni, msimu huu amecheza mechi nane za michuano yote.

Kiungo huyu aliivutia Liverpool kutokana na kiwango alichoonyesha msimu wa 2023/24 na aliisaidia Leverkusen kushinda taji la Bundesliga msimu huo.

Hata hivyo, kijana huyo, 22 hajang’aa tangu atue England na sasa ameonekana kupoteza nafasi kidogo kidogo chini ya Slot na alianzia benchi katika mchezo dhidi ya Everton ambao ulimalizika kwa Liverpool kushinda mabao 2-1.

Roo 01

Alianza  kwenye kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Crystal Palace ugenini, alionekana kuwa katika kiwango kibovu. Alitolewa dakika ya 74 na nafasi yake kuchukuliwa na Federico Chiesa.

Hadi sasa, Wirtz hajafunga bao wala kutoa asisti katika mechi zake nane za michuano yote alizocheza tangu kuanza kwa msimu huu.

Zaidi ya yote, amekuwa akitolewa kila mara anapoanza mechi, jambo linaloibua maswali juu ya nafasi yake na gharama zilizotumika kumnunua.

“Imekuwa ngumu kwake, sidhani kama kuna ubishi hapo anaonekana  anajitafuta kujaribu kurudi katika kiwango chake, unajua timu inaposajili wachezaji wengi wa kiwango cha juu, mara zote huwa wanajaribu kushindana na inavyoonekana Wirtz ameshindwa kuendana na kasi ya timu, ana uwezo mkubwa sana lakini mimi sioni kama ana nafasi ya kucheza katika kikosi,” alisema Rooney na kuongeza,

Roo 02

“Pesa iliyotumika ilikuwa ni nyingi sana na kwa mtazamo wangu Wirtz badala ya kusaidia, yeye anaharibu uwiano wa jinsi Liverpool inavyocheza. Lakini ni mchezaji mkubwa na nina hakika ataimarika siku za usoni, ni vile amekuwa na mwanzo wa kusuasua na hilo halina ubishi.” “Nimeona wachezaji wakija ligi hii na inachukua muda kwao kufanya vizuri. Kwa upande wangu, kinachomwangusha Wirtz si bei ya usajili, si uwezo wake bali ni aina ya sehemu ambayo anacheza anaonekana kutozoea zaidi kwani inamtaka muda mwingi kutengeneza mashambulizi na kucheza kwa chini kidogo tofauti na ilivyokuwa Leverkusen ambako alipewa uhuru wa kucheza

Katika mahojiano na Sky Germany hivi karibuni, Wirtz mwenyewe alikiri anakumbana na wakati mgumu.

“Bila shaka ningependa kuwa nimefunga bao au kutoa asisti hadi kufikia sasa, lakini haijalishi watu wanasema nini, sijipi presha sana. Sipendi kusikia kila mara ‘mpe muda, mpe muda.’ Badala yake, ninajaribu kufanya vizuri zaidi kila mara kuliko mwanzo. Naelewa wakati mwingine mambo hayaendi sawa. Sikuwahi kupitia hali kama hii mara nyingi katika kazi yangu lakini huwa inatokea.”