Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ukweli wa dili la Wirtz Liverpool

WITZ Pict

Muktasari:

  • Lakini, ada yote hiyo italipwa huko Bayer Leverkusen kama tu kikosi hicho cha Liverpool chini ya Kocha Arne Slot kitapata mafanikio makubwa wakati kikiwa na huduma ya kiungo Wirtz.

LIVERPOOL, ENGLAND; KIUNGO Florian Wirtz ametua Liverpool kwa ada iliyovunja rekodi ya uhamisho huko England ya Pauni 116 milioni, Juni mwaka huu.

Lakini, ada yote hiyo italipwa huko Bayer Leverkusen kama tu kikosi hicho cha Liverpool chini ya Kocha Arne Slot kitapata mafanikio makubwa wakati kikiwa na huduma ya kiungo Wirtz.

Huko nyuma, ada ya uhamisho iliyokuwa ikishikilia rekodi kwenye klabu ya Liverpool ni Pauni 85 milioni iliyolipwa kumsajili Darwin Nunez mwaka 2022. Lakini, baada ya hapo, Liverpool imevunja rekodi nyingine kwenye usajili, ilipomsajili straika Alexander Isak kwa Pauni 130 milioni.

Hata hivyo, kuhusu Pauni 116 milioni ya Wirtz, Pauni 100 milioni tu ndizo zenye uhakika wa kulipwa. Bosi wa usajili wa Liverpool, Richard Hughes kwenye dili hilo la Wirtz ni ada hiyo ya Pauni 100 milioni italipwa kwa awamu tano, Pauni 20 milioni kila awamu.

Hizo Pauni 16 milioni za ziada, Liverpool italipa huko Leverkusen kama tu miamba hiyo ya Anfield itapata mafanikio makubwa uwanjani.

Ripoti zinafichua mafanikio hayo ni kama Liverpool itabeba ubingwa wa Ligi Kuu England au Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa na huduma ya Wirtz kwenye kikosi chao.

Kiungo huyo Mjerumani baada ya kutua Liverpool alisaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Pauni 195,000 kwa wiki.

Wirtz alianzishwa kwenye mechi zote tatu ilizocheza Liverpool kwenye Ligi Kuu England hadi sasa, pamoja na ile ya Ngao ya Jamii. Kiungo huyo mchezeshaji ameasisti mara moja kwenye ya Ngao ya Jamii, lakini bado hajafunga wala kuchangia bao kwa mchezaji mwenzake kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.