Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Southgate aanza kutajwa Man United, mwenyewe afunguka

KUTAJWA Pict

Muktasari:

  • Southgate yuko tayari kukaa mezani na mabosi wa klabu hiyo, endapo watafikia uamuzi wa kuachana na kocha wa sasa Ruben Amorim, ambaye anakabiliwa na changamoto ya kupata matokeo mazuri.

ALIYEKUWA kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Sir Gareth Southgate anahofia atakosa muda wa kutosha kukifanyia mabadiliko kikosi cha Manchester United, endapo uongozi wa klabu hiyo utafanya uamuzi wa kumkabidhi benchi la ufundi kama kocha wao mpya.

Southgate yuko tayari kukaa mezani na mabosi wa klabu hiyo, endapo watafikia uamuzi wa kuachana na kocha wa sasa Ruben Amorim, ambaye anakabiliwa na changamoto ya kupata matokeo mazuri.

Vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa Southgate, ambaye ni shabiki wa muda mrefu wa Manchester United tangu utotoni, anaamini inaweza kuchukua hadi miaka minne kuifanya United kuwa wapinzani wa kweli katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Southgate pia ana wasiwasi kuwa United itahitaji mafanikio ya haraka hasa ikiwa ataonyesha maendeleo ya mapema ilhali yeye ni muumini wa mabadiliko ya taratibu na ya muda mrefu.

KUTA 01

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55, hana haraka ya kurejea kwenye kazi ya ukocha baada ya kujiuzulu kama kocha wa England mnamo Julai 2024.

Mwezi ujao, Southgate atatoa hotuba mbili huko London na York kwa ajili ya kutangaza kitabu chake kipya, Dear England: Lessons in Leadership, pia anahusika na miradi mingine nje ya soka. Southgate pia ameashiria kuwa huenda asifundishe tena.

Southgate ambaye aliwahi kuwa kocha wa Middlesbrough, ameendelea kuhusishwa na nafasi ya ukocha Manchester United tangu Sir Jim Ratcliffe alipokuwa mmiliki mwenza wa klabu hiyo mnamo Februari 2024.

KUTA 02

Ratcliffe alimteua bingwa wa mbio za baiskeli, Sir Dave Brailsford, kuongoza mageuzi ndani ya klabu hiyo, huku ikifahamika kiongozi huyo ana uhusiano wa karibu na Southgate.

Aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa United, Dan Ashworth, aliwahi kumpendekeza Southgate, baada ya kufanya naye kazi kwenye timu ya taifa ya England, kama chaguo bora la kumrithi Erik ten Hag mwaka jana. Hata hivyo, alipingwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Omar Berrada, ambaye alimuajiri Amorim.  

Brailsford ndiye aliyempendekeza Ashworth, lakini alidumu kwa miezi mitano pekee kama mkurugenzi wa michezo kabla ya kutimuliwa kutokana na kile Ratcliffe alikitaja kama alikosa wa ushirikiano.

Brailsford, ambaye aliwahi kuwa mkuu wa Team Sky, kwa sasa hayupo tena Manchester United na amerudi kwenye mbio za baiskeli kama Meneja Mkuu wa Ineos Grenadiers. Hata hivyo, jina lake bado linapatikana kwenye orodha ya wakurugenzi wa bodi ya soka ya United.