Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United yamweka katika rada zake Harry Kane

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Inaelezwa Kane ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka mwisho wa msimu kwa Pauni 57 milioni.

MANCHESTER United inafanya mpango wa kumsajili straika wa Bayern Munich, Harry Kane, 32, dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Inaelezwa Kane ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka mwisho wa msimu kwa Pauni 57 milioni.

Kane ambaye ni nahodha wa England, tayari amefunga mabao manne kwenye mechi nne msimu huu na kwa mujibu wa kipengele kilichopo katika mkataba wake anaweza kuuzwa ikiwa tu ataweka wazi nia yake ya kuachana na mabingwa watetezi wa Bundesliga, Januari mwakani.

Taarifa kutoka gazeti la  Kijerumani Bild, Kane, 32 ana hamu kubwa ya kurejea England baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026 na Man United ni miongoni mwa timu ambazo zipo tayari kumchukua kwa wakati huo.

Man United inadaiwa kutamani huduma ya Kane kwani licha ya kusajili washambuliaji katika dirisha lililopita bado hawajaonyesha kiwango kilichotarajiwa.


Kobbie Mainoo

KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo, 20, anajiandaa kuondoka Januari mwakani kujiunga na timu nyingine itakayompa nafasi kubwa ya kucheza tofauti na ilivyo sasa akiwa na Man United. Awali katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi  Man United ilikataa kumtoa kwa mkopo licha ya kuwasilishwa kwa ofa kutoka timu kibao za England na nje ya nchi hiyo. Mkataba wa sasa wa Mainoo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Michael Olise

BAYERN Munich inataka kumsainisha mkataba mpya winga wao wa kimataifa wa Ufaransa, Michael Olise na tayari imeshampa ofa ya mkataba mpya na sasa mazungumzo yanaendelea. Olise mwenye umri wa miaka 23, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029, msimu uliopita alicheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao saba. Kocha Vincent Kompany amevutiwa sana na kiwango chake.


Kenan Yildiz

ARSENAL imefanya mawasiliano na Juventus kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo, Kenan Yildiz, 20, dirisha lijalo la majira ya baridi Januari. Chelsea ilijaribu kuwasilisha ofa kumsajili dirisha lililopita la majira ya kiangazi lakini ilishindikana baada ya Juve kuikataa. Kuna uwezekano mkubwa Juventus ikakubali kumuuza ikiwa timu inayomhitaji itawasilisha ofa isiyopungua kati ya Pauni 70 hadi 87 milioni.


Ismael Doukoure

CHELSEA inataka kumsajili beki kisiki wa Strasbourg, Ismael Doukoure, 22, dirisha lijalo la majira ya baridi kwa ajili ya kuboresha zaidi eneo lao la uzuiaji. Timu nyingi za Ligi Kuu England lakini Chelsea ina matumaini makubwa zaidi ya kumsajili Doukoure kwa sababu wamiliki wao ndio wamiliki wa Strasbourg. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu uliopita alicheza mechi sita za michuano yote.


Jadon Sancho

ASTON Villa inataka kumsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Jadon Sancho ambaye anacheza katika kikosi chao kwa mkopo. Sancho alijiunga na Villa katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi baada ya kocha Ruben Amorim kutomhitaji katika kikosi chake. Mkataba wa sasa wa Sancho unatarajiwa kumalizika mwakani.


Ryan Gravenberch

LIVERPOOL imefikia hatua nzuri katika mazungumzo yao ya kumsainisha mkataba mpya kiungo wao wa kimataifa wa Uholanzi, Ryan  Gravenberch mwenye umri wa miaka 23. Mkataba wa sasa wa Ryan unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na Liverpool inapambana kumsainisha mkataba mpya kutokana na kiwango alichoonyesha akiwa katika kikosi chao.


Takefusa Kubo

ARSENAL imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili winga wa Real Sociedad, Takefusa Kubo dirisha lijalo la majira ya baridi. Kubo, 24, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Sociedad na msimu huu amecheza mechi sita za michuano yote. Mabosi wa Sociedad wanahitaji Pauni 40 milioni kwa ajili ya kumuuza staa huyu.