Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LeBron James afikia uamuzi mgumu

JAMES

Muktasari:

  • Mwandishi wa NBA, Chris Haynes, amefichua kuwa amezungumza na wakala wa LeBron, Rich Paul, ambaye amethibitisha kuwa sasa kila kitu kipo mikononi mwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 41.

LOS ANGELAS, MAREKANI: SAFARI ya mkongwe LeBron James kuelekea msimu mpya wa NBA imeingia hatua ya mwisho, huku ikielezwa kuwa tayari ana taarifa zote muhimu zinazohitajika kabla ya kufanya uamuzi wa timu atakayoichezea.

Mwandishi wa NBA, Chris Haynes, amefichua kuwa amezungumza na wakala wa LeBron, Rich Paul, ambaye amethibitisha kuwa sasa kila kitu kipo mikononi mwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 41.

"Nimezungumza na Rich Paul na ameniambia LeBron tayari ana taarifa zote muhimu. Sasa kinachosubiriwa ni uamuzi wake," amesema Haynes kupitia kipindi cha NBA Prime.

JAME 01

TIMU TANO ZAMUWANIA

Kwa sasa, timu tano ndizo zinazopewa nafasi kubwa ya kupata saini ya LeBron endapo ataondoka.

Ya kwanza ni Cleveland Cavaliers, Miami Heat, Golden State Warriors, Philadelphia 76ers na Minnesota Timberwolves.

Awali kulikuwa na tetesi za New York Knicks, lakini taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo imejiondoa kwenye mbio hizo.

JAME 02

SI PESA, BALI FURAHA

Rich Paul amesema tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma, LeBron hana tena shinikizo la kutafuta ubingwa mwingine kwa gharama yoyote.

Badala yake, anataka kujiunga na timu yenye mazingira mazuri ya ushindani na mfumo wa mchezo unaomfaa.

"LeBron ataweka furaha na ustawi wake mbele kuliko fedha. Anataka mradi wa michezo unaomfaa na unaompa nafasi ya kufurahia mchezo."

Aidha, Paul amesisitiza kuwa endapo familia yake, hasa mke wake Savannah na binti yake Zhuri, watampa baraka, LeBron yuko tayari kusaini mkataba wa zaidi ya msimu mmoja badala ya makubaliano ya muda mfupi.

JAME 03

UAMUZI WATARAJIWA WIKI HII

Ripoti zinaeleza kuwa LeBron anaweza kutangaza rasmi uamuzi wake katika tamasha la Fanatics Fest 2026 litakalofanyika jijini New York.