Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bernardo Silva kuwafuata Ronaldo, Felix Saudi Arabia

SILVA Pict

Muktasari:

  • Silva amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Man City tangu ajiunge nacho mwaka 2017 akiitumikia kama kiungo mshambuliaji lakini tangu msimu uliopita amekuwa akiwindwa na vigogo wengi kutoka Saudi Arabia ambao wapo tayari kumpa zaidi Pauni 500,000.

KIUNGO wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Bernardo Silva, 31, amepanga kutimkia Saudi Arabia dirisha lijalo la majira ya kiangazi kuungana na nyota wenzake wa Ureno, Cristiano Ronaldo na Joao Felix na mkataba wake utakuwa unamalizika.

Silva amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Man City tangu ajiunge nacho mwaka 2017 akiitumikia kama kiungo mshambuliaji lakini tangu msimu uliopita amekuwa akiwindwa na vigogo wengi kutoka Saudi Arabia ambao wapo tayari kumpa zaidi Pauni 500,000.

Al Hilal imeweka mezani ofa hiyo ya mshahara wa Pauni 500,000 kwa wiki na bonasi ya usajili ya Pauni 2 milioni.  Inaelezwa Silva alikataa kwenda Saudia awali kwa sababu alihitaji kuendelea kucheza soka la kiushindani ili kuwepo kikosi cha Ureno kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwakani.

Hadi sasa amecheza zaidi ya mechi 400 akiwa na Man City. Msimu uliopita alicheza mechi 10 za michuano yote na kufunga bao moja.


Dusan Vlahovic

MANCHESTER United inatamani kumsajili mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Serbia, Dusan Vlahovic, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha la usajili la Januari.  Vlahovic ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na Juventus tangu msimu uliopita na vigogo mbalimbali kutoka England wamekuwa wakiinyemelea saini yake na mbali ya Man United, Chelsea pia inamhitaji. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.


Joao Neves

KIUNGO wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ureno, Joao Neves, mwenye umri wa miaka 21, ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na  Manchester City ambayo inataka kuwasilisha ofa mwisho wa msimu huu. Hata hivyo, PSG inamwangalia fundi huyu kama staa tegemeo katika mipango yao na haina mpango wa kukubali ofa kutoka timu yoyote. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.



Julian Alvarez

LIVERPOOL huenda ikajiondoa katika mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, 25, kutokana na kiasi kikubwa cha pesa ambacho timu yake inakihitaji ili kumuuza. Kwa mujibu wa ripoti, Atletico imeanzia kudai Pauni 100 milioni ambayo Liverpool inaamini hata ikifanya mazungumzo na kuomba kushushiwa itafikia Pauni 80 hadi 70 milioni wanayoiona bado ni nyingi.


Moises Caicedo

REAL Madrid wanawafuatilia kwa karibu viungo wa kati wa Chelsea, Enzo Fernandez, 24, na Moises Caicedo, 23. Wababe hao wa Hispania wamepanga kusajili mmoja kati yao na inaonekana wanahitaji sana huduma ya Caicedo ambaye ameendelea kuwa na kiwango bora tangu ajiunge na Chelsea akitokea Brighton. Hivi karibuni Fernandez  amekuwa na kiwango cha chini hali iliyowarudisha nyumba vigogo hao.


Fikayo Tomori

AC Milan imeanza mazungumzo na wawakilishi wa beki wao raia wa  England, Fikayo Tomori, mwenye umri wa 27, kuhusu kumwongeza mkataba mpya baada ya kuona timu nyingi hususan zile za England zimeanza kumnyemelea. Tomori amekuwa akifanya vizuri katika Serie A akiwa AC Milan na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Gustavo Prado

MASKAUTI wa Leeds United wanaendelea kumchunguza kiungo wa kati raia wa Brazil, Gustavo Prado, 20, ambaye inataka kumsajili Januari mwakani. Klabu yake ya sasa, Internacional, inahitaji ada ya uhamisho ya takribani Pauni 17 milioni ili kumuuza staa huyo ambaye msimu uliopita alicheza mechi 22 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.


Takefusa Kubo

ARSENAL itawasilisha ofa ya Euro 75 milioni kwenda  Real Sociedad  kwa ajili ya kusajili wachezaji wawili kutoka timu hiyo. Mastaa wanatajwa kuwa ni winga wa kimataifa wa  Japani, Takefusa Kubo, mwenye umri wa  miaka 24, na beki kutoka Ufaransa Lucien Agoume, mwenye miaka 23.  Kubo, aliyewahi kuwa mali ya Real Madrid, ameng’ara sana La Liga akiwa na Sociedad tangu msimu uliopita.