Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bernardo Silva aipa ubingwa Liverpool, Arsenal

UBINGWA Pict

Muktasari:

  • Silva alijiunga na Man City mwaka 2017 na tangu muda wote huo ni misimu miwili tu ndio alimaliza bila ya kuvaa medali ya ubingwa wa EPL.

MANCHESTER, ENGLAND: FUNDI wa boli, Bernardo Silva amekiri kwamba nafasi ya Liverpool na Arsenal kushinda Ligi Kuu England kwa sasa ni kubwa zaidi kuliko ya Manchester City.

Silva alijiunga na Man City mwaka 2017 na tangu muda wote huo ni misimu miwili tu ndio alimaliza bila ya kuvaa medali ya ubingwa wa EPL.

Liverpool iliipiku Man City kushinda ubingwa mwaka 2020 kabla ya kushinda tena ubingwa msimu uliopita ikiwa na kocha mpya Arne Slot.

Baada ya kutawala kwa muda mrefu, Man City ilijikuta katika nyakati ngumu msimu uliopita ingawa ilifanikwa kumaliza ndani ya nafasi tatu za juu.

Licha ya kuishinda Manchester United kwa mabao 3-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, matumaini ya Man City ya kuchukua ubingwa yamepungua kutokana na kupoteza kwa mabao 2-0, mbele ya Tottenham nyumbani pamoja na kupoteza dhidi ya Brighton kwa mabao 2-1 ugenini.

Kutokana na kiwango ambacho Arsenal na Liverpool zimeonyesha tangu kuanza kwa msimu huu, Silva anaamini kwamba Man City haina nafasi kubwa ya kushinda Ligi Kuu England.

"Naweza kusema Liverpool na Arsenal ndio zina nafasi za kushinda taji ingawa bado ni mwanzo, hivyo ni mapema kusema kwa sababu hata msimu uliopita watu walitoa utabiri wao na kusema Manchester City na Arsenal zinaweza kushinda taji na Liverpool haikuwa inapewa nafasi, lakini bado ilishinda Ligi Kuu. Mwanzoni huwezi kufanya hesabu nyingi.

"Kwa hakika, tunaweza kuzungumza kuhusu timu yetu na kusema kwamba kiwango chetu bado sio kile tunachotaka, lakini tunajua kwamba tukifikia kiwango hicho, hakuna timu nyingi zinazoweza kutuzuia.

"Unajua katika ligi hii, hata kama unaongoza kufikia Februari huwezi kuwa na uhakika wa kuchukua ubingwa, lakini unaweza kujua kama umeupoteza kufikia wakati huo. Tunachotaka ni kurudi kwenye kiwango chetu kufikia pale tunapotaka."

Msimu huu Man City imeimarisha kikosi chake kwa kuwasajili Tijjani Reijnders, Rayan Ait-Nouri, Rayan Cherki, James Trafford na Gianluigi Donnarumma, ambao waligharimu takribani Pauni 170 milioni.

Vilevile ilitumia Pauni 175 milioni katika dirisha la usajili la Januari mwaka huu, kukamilisha sajili za Omar Marmoush, Nico Gonzalez, Abdukodir Khusanov na Vitor Reis.

Hata hivyo, gharama ya Liverpool katika dirisha la majira ya kiangazi ilikuwa kubwa zaidi kuzidi kiasi ambacho Man City imekitumia tangu kuanza kwa mwaka huu.

Liverpool imefanikiwa kuwasajili Alexander Isak, Florian Wirtz, Hugo Ekitike, Milos Kerkez, Jeremie Frimpong na Giovanni Leoni kwa takriban Pauni 446 milioni.

Kabla ya mchezo wao wa jana dhidi ya Arsenal, Man City ilikuwa inashika nafasi ya 12 kwa pointi sita baada ya mechi nne.