Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arne Slot ‘amtibua’ gwiji Liverpool

GWIJI Pict
GWIJI Pict

Muktasari:

  • Carragher amesema Liverpool inacheza kama sio timu ya kiwango cha juu na inapokuwa kiwanjani ni vurugu tupu.

LIVERPOOL, ENGLAND: LEJENDI wa Liverpool, Jamie Carragher amemshambulia vikali kocha wa timu hiyo Arne Slot na wachezaji wake baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo, akisisitiza kwamba wanacheza kama timu ndogo.

Carragher amesema Liverpool inacheza kama sio timu ya kiwango cha juu na inapokuwa kiwanjani ni vurugu tupu.

Liverpool ilipoteza mechi ya pili mfululizo baada ya kuchapwa bao 1-0 na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya jana.

Bao pekee la mechi hiyo iliyopigwa jijini Istanbul, liliwekwa wavuni na straika Mnigeria, Victor Osimhen kwa mkwaju wa penalti katika kipindi cha kwanza.

Majogoo hawa wamepata kipigo hicho siku tatu tu baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu England.

"Sihisi kama ninaangalia timu kubwa ikiwa inacheza. Liverpool kwa sasa haichezi soka, wanacheza kama wapo katika mpira wa kikapu, yaani wakipata mpira ni kwenda kwa timu pinzani tu, hakuna mipango. Sidhani kama timu kubwa hucheza namna hiyo," amesema Carragher alipokuwa akichambua mchezo huo kupitia CBS Sports.

SLO 01

Hata hivyo, kabla ya kuanza kupoteza dhidi ya Palace, Liverpool ilikuwa imeshinda mechi zote saba za mwanzo katika mashindano yote msimu huu na inaongoza Ligi Kuu England ikiwa pointi mbili mbele ya Arsenal.

Carragher amesema timu hiyo haikuwa inacheza vizuri hata wakati ilipokuwa ikishinda katika mechi hizo saba.

"Sio kuhusu kupoteza, wala si kuhusu matokeo, bali ni kiwango cha mchezo. Hii imekuwa ikijionyesha tangu siku ya kwanza. Liverpool ilichezwa vizuri sana na Newcastle hususani kipindi cha pili, Palace mwishoni mwa wiki ilitengeneza nafasi saba kubwa za kufunga mabao, idadi ambayo hakuna timu nyingine imewahi kutengeneza msimu huu na kumbuka, Liverpool ndio mabingwa. Kwa hiyo haya matokeo hayanishangazi, na kocha lazima arekebishe hali hii haraka."

Liverpool itacheza mechi inayofuata Jumamosi dhidi ya Chelsea katika Ligi Kuu England ambayo inatarajiwa kuwa ngumu kwao hususani katika kipindi hiki ambapo inaonekana kusuasua.

Kwa upande wake kocha wa Liverpool, Arne Slot, amesema timu yake ilizidiwa ujanja na Galatasaray jambo lililosababisha kupoteza mechi hiyo.

SLO 02

Slot amesema: "Winga wa Galatasaray, Baris Yilmaz alihisi tu kama kapigwa kidogo usoni, akaanguka chini mara nyingi na kuzawadiwa penalti. Siwezi kumlaumu Dom (Szoboszlai, aliyesababisha penalti) kwa hali tukio hili. Wamegeuza penalti ya asilimia 20 kuwa ya asilimia 100."

Licha ya kukubali kichapo Liverpool pia ilipata pigo la majeruhi baada ya kipa wao Alisson Becker na straika Hugo Ekitike kuumia na kulazimika kutolewa na ripoti zinadai Becker hatakuwapo katika mechi ya wikiendi hii.