Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo CAF kukutana leo Morocco kujadili CAF Super League

Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) inatarajia kukutana leo huko Rabat, Morocco kuanzia saa 1 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki.

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya CAF kitakuwa chini ya uongozi wa mwenyekiti wake, Dk. Patrice Motsepe ambaye ni Rais wa chombo hicho cha juu cha uongozi wa mpira wa miguu Afrika.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa na kutolewa uamuzi katika kikao hicho ni uanzishwaji wa mashindano ya 'CAF Super League' ambayo yamezua mjadala mkubwa kwa wadau na mashabiki wa mpira wa miguu Afrika.

Wazo la kuanzishwa kwa mashindano hayo lilianzishwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino mara baada ya mpango huo kukwama barani Ulaya.

Lakini ukiondoa agenda hiyo, nyingine ambayo ina uzito ni ile ya kujadili ripoti ya ukaguzi wa fedha na utekelezaji wa mipango ya CAF ijulikanayo kama PricewaterhouseCoopers (PwC)

Ripoti hiyo inasubiriwa kwa hamu kwani kihistoria ndizo zimekuwa zikiibua skendo na taarifa za madudu kwa watendaji wa CAF hasa matumizi mabaya ya ofisi, makosa ya rushwa na ubadhilifu.

Kumekuwepo na taarifa za ufujaji wa fedha na matumizi mabaya ya ofisi ambayo yamekuwa yakifanywa na baadhi ya watendaji wa CAF na hivyo ripoti hiyo huenda ikawakaanga baadhi yao.