Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbio za Saifee kusaidia Wanawake

JANA jijini Dar es Salaam zilifanyika mbio maalumu kwaajili ya kuchangia matibabu ya saratani ya matiti kwa wanawake.

Mbio hizo zilizoandaliwa na Hospital ya Saifee, ziligawanywa kwa kilometa tano, 10 na 21 zikianzia uwanja wa Farasi na kumalizikia hapo.

Mgeni rasmi kwenye mbio hizo alikuwa Naibu Waziri wa Afya Godwin Mollel ambaye aliupongeza uongozi wa Saifee na kutaka wananchi waendelee kutumia michezo  kusaidia sekta na maeneo mengine mbali mbali.

“Leo kupitia michezo (mbio), Wanawake wenye saratani ya Matiti wanaenda kupata matibabu. Hii ni njia nzuri na niwahimize muendelee kutumia michezo katika mambo chanya kama haya.

Serikali tupo tayari kuunga mkono juhudi za taasisi binafsi ili kuleta maendeleo. Wanawake wengi wamekuwa wakipata shida ya Saratani ya Matiti na kwa kiasi  flani matibabu yao ni gharama hivyo tuendelee kusaidiana kila tunapopata nafasi,” alisema Mollel.

Nje ya Mollel, katika mbio hizo walikuwepo pia, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Hafidhi na viongozi wengine wengi wa Serikali.

Mkurugenzi mtendaji wa Saifee, murtaza Aymal alisema fedha zitakazopatikana zitaenda kusaidia Wanawake wengi katika matibabu.

“Lengo ni kusaidia Wanawake kupata matibabu stahiki ya kuna changamoto kubwa ya Saratani ya Matiti na uponyaji wake hivyp tumeamua kutumia mbio ili watu wa kada mbali mbali wajitokeze kuchangia na kusaidia katika hilo,” alisema Murtaza.