Washindi Betika mtoko wa Kibingwa watua Dar
Muktasari:
- Hiyo ni mara ya pili kwa washindi wa Betika mtoko wa kibingwa kupewa fursa hiyo, awali ilikuwa mwaka jana kwenye moja ya mechi ya Yanga na Simba.
Washindi kwenye promosheni ya Betika Mtoko wa Kibingwa iliyotoa fursa kwa mashabiki 24 wa Simba na Yanga kushuhudia mchezo wa dabi, wamewasili jijini Dar es Salaam leo tayari kuungana na mashabiki wengine kushuhudia mchezo huo wa dabi kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Mkapa.
Mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam wakitokea mikoa mbalimbali nchini, washindi hao ambao ni wanazi wa timu hizo walitambiana baadhi wakiweka kete kwa Yanga na wengine wakiipa nafasi Simba kuondoka na pointi tatu kesho.
Meneja Masoko wa kampuni ya Betika, Nelson Mwanuzi amesema washindi wote wamewasili leo na kesho watakuwa miongoni mwa mashabiki watakaoshuhudia dabi hiyo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, Tanzania Bara kwa udhamini wa Betika.
"Wote wamegharamiwa na Betika, watashuhudia mechi hiyo kwa hadhi ya VIP, kuanzia wakiwa hoteli hadi uwanjani na wataondoka Dar es Salaam Jumapili," amesema Mwanuzi.
Baadhi ya washindi wameishukuru kampuni ya Betika kwa kuwapa fursa ya kushuhudia mechi hiyo ya dabi huku baadhi yao wakifichua kuwa ni mara yao ya kwanza kwenda Dar es Salaam kushuhudia dabi hiyo laivu.
Sharafi Sharkati wa Mtwara amesema Betika imempa fursa ya kuja kushuhudia dabi hiyo ambayo mbali na kuwa mechi ya heshima, matokeo mazuri ni muhimu kwa timu zote mbili.
"Japo natamani Yanga ishinde, lakini Betika imeweka historia mpya kwangu kwenye soka kwa kuwa miongoni mwa washindi wa Mtoko wa Kibingwa," amesema.
Hamis Omary wa Tabora amesema anaamini mechi itakuwa na upinzani na nzuri na dakika 90 ndizo zitaamua matokeo.
Washindi wengine wa Betika Mtoko wa Kibingwa ni Mbaraka Selemani wa Mtwara, Justine Bulaya wa Arusha, Sifa Kaminyoge wa Mbeya, Lameck Ndimugangwe na Edward Zakayo wa Kigoma, Peter Martin wa Singida, Leopord Thobias na Masatu John wa Mwanza.
Wengine ni Dismas Chiloloma wa Dodoma, Aaron Kulinga wa Mbeya, Emmanuel Kivambe wa Shinyanga, Boniface Molel wa Manyara, Shafii Mgomi Mtwara na Raphael Kibifu wa Tabora.
Wengine ni Emmanuel Zadie na Amos Mdao wa Dodoma, Sharafi Sharkati wa Mtwara, Michael Richard, Patrick Ngwala na Ibrahim Kondo wa Morogoro, Dominick Mwakalinga wa Mbeya, Lameck Mbusiro wa Mara, Hamis Omary wa Tabora na Furaha Juma wa Sumbawanga.