Messi: Kutoka winga mwenye kasi hadi mfalme wa soka la akili
Muktasari:
- Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 39 ameendelea kuthibitisha ubora wake katika Kombe la Dunia la sita, akiweka rekodi ya kuch eza mara nyingi zaidi sambamba na Cristiano Ronaldo wa Ureno na Guillermo Ochoa wa Mexico. Mpaka sasa Messi ameifungia Argentina mabao nane na kutoa pasi tano za mabao, akiongoza mbio za Kiatu cha Dhahabu pamoja na Kylian Mbappe wa Ufaransa.
DALLAS, MAREKANI: IWAPO Argentina itafanikiwa kutetea ubingwa wa Kombe la Dunia 2026, jambo ambalo halijawahi kufanywa na taifa lolote tangu Brazil mwaka 1962, basi jina la Lionel Messi litakuwa kiini cha mafanikio hayo.
Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 39 ameendelea kuthibitisha ubora wake katika Kombe la Dunia la sita, akiweka rekodi ya kuch eza mara nyingi zaidi sambamba na Cristiano Ronaldo wa Ureno na Guillermo Ochoa wa Mexico. Mpaka sasa Messi ameifungia Argentina mabao nane na kutoa pasi tano za mabao, akiongoza mbio za Kiatu cha Dhahabu pamoja na Kylian Mbappe wa Ufaransa.
Lakini safari hii dunia inaiona sura tofauti ya Messi. Si yule kijana mwenye kasi aliyetikisa Barcelona mwaka 2003, bali ni mchezaji aliyebadilisha kabisa namna ya kucheza ili aendelee kutawala soka la dunia.
ENGLAND YAKUTANA NA MESSI MPYA
Jumatano hii, Argentina itakutana na England katika nusu fainali ya Kombe la Dunia, mechi ambayo Messi alithibisha ubora wake kwa kutoa asisti mbili katika ushindi wao wa mabao 2-1 nakutinga fainali. Tofauti na nyota wengi wanaopungua kiwango wanavyozeeka, Messi amebadilisha mchezo wake badala ya kushindwa na umri.
SASA ANAKIMBIA KIDOGO LAKINI ANA FIKIRI HARAKA ZAIDI.
Katika Kombe hili la Dunia, ametembea kwa asilimia 47 ya umbali wote aliotumia uwanjani, kiwango cha juu kuliko mchezaji yeyote wa nafasi ya uwanjani.
Pia amekuwa akikimbia wastani wa kilomita 8.2 pekee kwa kila dakika 90, idadi ndogo zaidi kwa wachezaji wa Argentina waliocheza dakika nyingi.
Amefanya wastani wa mbio fupi (sprints) 2.7 kwa mechi, ikilinganishwa na 5.3 alizokuwa akifanya miaka minne iliyopita.
Hata hivyo, takwimu hizo hazijazuia ubora wake.
Messi amepiga mashuti 33 na kutengeneza nafasi 21 za mabao katika mashindano haya, jumla ya matukio 54 ya kushambulia, idadi kubwa zaidi tangu Diego Maradona alipofanya hivyo mwaka 1986.
Katika mechi 15, Messi amehusika moja kwa moja kwenye mabao 23, akifunga 16 na kutoa asisti saba.
GUARDIOLA ALIYEBADILI HISTORIA YA MESSI
Mwanzoni mwa maisha yake Barcelona, Messi alikuwa winga wa kulia aliyependa kupenya na kukata kuelekea katikati.
Lakini mwaka 2009, kocha Pep Guardiola alifanya uamuzi uliobadili historia ya soka. Alimtoa pembeni na kumchezesha kama False Nine, nafasi ambayo haikuwa mshambuliaji wa kawaida bali mchezaji huru anay eshuka katikati kutengeneza nafasi.
Jaribio hilo lilianza katika ushindi wa kihistoria wa Barcelona wa mabao 6-2 dhidi ya Real Madrid Santiago Bernabeu.
Kuanzia hapo, mabeki walishindwa kuelewa wamfuate au wabaki kwenye nafasi zao, na Messi akaanza kutawala mechi kwa akili badala ya kasi.
Ndani ya misimu miwili iliyofuata alifunga mabao 96 katika mechi 69 za La Liga na kuanza kutawala tuzo za Ballon d’Or.
Messi mwenyewe aliwahi kusema:
“Nilijifunza mengi kutoka kwa Guardiola. Alinifundisha kuelewa nafasi, kutunza mpira na jinsi mchezo unavyofanya kazi.”
Kutoka mfungaji hadi mtengeneza mchezo
Baada ya Xavi Hernandez na Andres Iniesta kuondoka Barcelona, Messi alibadilika tena.
Badala ya kusubiri mipira mbele, alianza kushuka chini kuanzisha mashambulizi, kutengeneza nafasi na bado kufunga.
Msimu wa 2019/20 alitoa asisti 22 na kufunga mabao 25 katika La Liga.
Hata alipohamia Paris Saint-Germain, alimaliza msimu wake wa kwanza akiwa na asisti nyingi (15) kuliko mabao (11), jambo lililoonyesha jinsi alivyobadilika kuwa mchezaji wa kutengeneza nafasi zaidi kuliko kumalizia.
ALIYEKUWA KIMYA AKAWA KIONGOZI, SAFARI YAKE NA ARGENTINA PIA ILIBADILIKA
Baada ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia 2014 na fainali mbili za Copa América mwaka 2015 na 2016, Messi aliwahi hata kutangaza kustaafu timu ya taifa.
Lakini alirejea akiwa mtu tofauti.
Mwaka 2021 aliiongoza Argentina kutwaa Copa America dhidi ya Brazil, kisha mwaka 2022 akatimiza ndoto ya kutwaa Kombe la Dunia.
Leo hii si tu mchezaji bora, bali ndiye kiongozi anayebeba matumaini ya taifa zima.
MESSI WA MWISHO NDIYE BORA ZAIDI
Akiwa Inter Miami na sasa kwenye Kombe la Dunia 2026, Messi anakimbia kidogo kuliko wakati wowote katika maisha yake.
Lakini kila anapogusa mpira, anaonekana kuona mchezo sekunde kadhaa kabla ya wengine.
Aliyekuwa kiungo na rafiki yake wa karibu, Pablo Aimar, aliwahi kusema:
“Messi wa mwisho ndiye Messi bora zaidi.”
Kauli hiyo inaonekana kuthibitishwa tena. Kutoka kijana aliyewashangaza mabeki akiwa Barcelona, hadi False Nine, baadaye mtengeneza mchezo, nahodha bingwa wa dunia na sasa mkongwe anayesoma mchezo kwa akili ya kipekee, Messi ameendelea kujibadilisha kila hatua ya maisha yake.
TAKWIMU ZA KIFALME
Dhidi ya England, Messi aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza tangu mwaka 1966 kufanikiwa kufanya kukokota mpira mara tisa ‘dribbling’ na kutoa asisti mbili katika mchezo mmoja wa hatua ya mtoano wa Ko mbe la Dunia. Cha kushangaza zaidi, England yote ilifanikiwa kufanya dribbling saba pekee katika mchezo mzima.
Messi pia alikuwa na miguso saba ndani ya eneo la hatari la England, idadi sawa na wachezaji wote wa England kwa pamoja. Aliunda nafasi nne za mabao, sawa pia na timu nzima ya England, huku akipiga krosi tisa zilizokuwa nyingi kuliko mchezaji mwingine yeyote uwanjani.
Kipa wa Argentina, Emiliano Martinez, alisema kumpeleka Messi upande wa kulia kulikuwa silaha yao kubwa.
“Kumhamishia Messi pembeni ndiyo kulibadili mchezo. Alitupa kile tulichokuwa tunahitaji,” alisema.
‘GOAT’ ANAENDELEA KUANDIKA HISTORIA
Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, hakusita kumsifu nahodha wake.
“Yeye ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea. Sijui bado anatakiwa kufanya nini ili watu waamini hilo. Wahispania wengi pia wanampenda.”
Mchambuzi wa BBC na beki wa zamani wa England, Micah Richards, alisema:
“Argentina ina Lionel Messi. Ina GOAT. Mchezaji bora kuliko wote. Hii ndiyo tofauti yake; ana uwezo wa kubadili mechi kwa muda mfupi.”
Nahodha wa England, Harry Kane, alikiri walifanikiwa kumzuia kwa muda mrefu, lakini ubora wake uliamua matokeo.
“Tulimdhibiti kwa sehemu kubwa ya mchezo, lakini wachezaji wa kiwango chake wanahitaji nafasi moja tu kubadili kila kitu. Ndiyo maana anahesabiwa miongoni mwa wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea.”