Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zion ajibu tuhuma za kuwakimbia watoto wake

ZION Pict

Muktasari:

  • Zion ambaye pia ni mchumba wa zamani wa mwimbaji Jesy Nelson, amevunja ukimya kuhusu kuachana kwao na kusisitiza kuwa ataendelea kuwalea mabinti wao mapacha.

Msanii wa R&B na Hip-hop kutoka Uingereza, Zion Foster ametoa ufafanuzi kuhusu malezi ya watoto wake wawili ambao awali ilidaiwa amekimbia kwenye malezi yao.

Zion ambaye pia ni mchumba wa zamani wa mwimbaji Jesy Nelson, amevunja ukimya kuhusu kuachana kwao na kusisitiza kuwa ataendelea kuwalea mabinti wao mapacha.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuzuka kwa taarifa zilizoonyesha kuwa alihisi kuzidiwa kutokana na mabinti wao, Ocean na Story, kugundulika kuwa na ugonjwa adimu wa Spinal Muscular Atrophy (SMA) Aina ya 1.

ZIO 03

Spinal Muscular Atrophy (SMA) ni ugonjwa wa kurithi unaoshambulia mishipa ya fahamu inayodhibiti misuli, na kusababisha misuli kudhoofika taratibu. Aina ya kwanza (Type 1), ambayo waliyo nayo mabinti wa Jesy Nelson na Zion Foster, huanza kujitokeza mtoto akiwa mchanga na inaweza kuathiri uwezo wa kukaa, kupumua na kumeza bila matibabu ya mapema.

Akifafanua kauli yake, Zion alisema aliposema alikuwa amezidiwa hakumaanisha kwamba alikuwa anakimbia majukumu yake ya ubaba, bali alikuwa akieleza hali halisi ya kushughulikia taarifa nzito za kiafya ambazo hakuwahi kukutana nazo awali.

ZIO 01

“Nilikuwa najifunza nilikuwa nikijaribu kuelewa hali hiyo. Hiyo haikumaanisha kwamba sikuwapenda watoto wangu au kwamba ningeacha kuwa baba yao,” alisema.

Mbali na hilo, Zion alidai kuwa uamuzi wa kuachana ulikuwa wa Jesy, lakini akaweka wazi kuwa mwisho wa mapenzi yao hauwezi kuwa mwisho wa wajibu wake kwa watoto wao.

“Ninahudhuria kila miadi yao ya hospitali, najifunza kuhusu ugonjwa wao kila siku na ninafanya kila niwezalo kuhakikisha ninakuwa sehemu ya maisha yao. Kuwa baba yao ni jambo kubwa zaidi maishani mwangu,” ameongeza.

ZIO 02

Kauli hiyo imekuja wakati Jesy akijiandaa kuzindua makala yake mpya ya Life Changing, ambayo inaonyesha safari yake na Zion baada ya mabinti wao kugundulika kuwa na ugonjwa huo.