Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu ya Zuchu kuomba talaka kwa Diamond Platnumz

ZUCHU Pict


BAADA ya miaka sita ya uhusiano uliogubikwa na furaha, migogoro, kuachana na kurudiana, hatimaye msanii wa WCB Wasafi, Zuchu, ametangaza kuachana na mumewe, Diamond Platnumz, huku wawili hao wakiendelea na mchakato wa talaka.


Tangazo hilo alilitoa Julai 12, 2026 katika ukurasa wake wa Instagram, Zuchu amesema umefika wakati wa kujichagua mwenyewe, kuanza kupona na kuelekeza nguvu zake kwenye afya pamoja na kazi zake.


"Mimi na aliyekuwa mwenzangu we are now separated and going through a divorce... After six years of being together I have finally decided to choose myself," aliandika Zuchu.

Kauli hiyo imeibua maswali mengi kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakiamini wawili hao walikuwa wamefanikiwa kuvuka changamoto nyingi zilizowahi kuikumba ndoa yao.

ZUCHU Pict

Madai yanayotajwa
Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata kutoka kwa watu wa karibu na wawili hao zinaeleza miongoni mwa mambo yanayotajwa ndani ya mgogoro huo ni changamoto za kutokuwa na uaminifu katika ndoa.

Ingawa madai hayo yamekuwa yakizungumzwa na watu wa karibu pamoja na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii, Mwanaspoti haikuweza kuyathibitisha kutoka kwa Diamond Platnumz wala Zuchu hadi wakati makala haya yanaandikwa.

Hata hivyo, jambo ambalo liko wazi ni kwamba, si mara ya kwanza suala hilo kuibuka.

Katika nyakati tofauti za uhusiano wao, Zuchu mwenyewe aliwahi kuandika katika akaunti zake za mitandao ya kijamii akilalamikia kile alichodai ni usaliti, huku pia akizungumzia maumivu aliyokuwa akiyapitia ndani ya uhusiano wao.

Kauli hizo ziliibua mjadala mkubwa na kufanya mashabiki wengi kuamini suala la uaminifu lilikuwa miongoni mwa changamoto zilizokuwa zikiusumbua uhusiano huo.

Pia Sababu nyingine inadaiwa familia ya Diamond Platnumz, kutokuwa na upendo mkubwa na Zuchu na kuwapa nafasi kubwa baadhi ya wanawake ambao Diamond Platnumz aliwahi kujihusisha nao kimapenzi.

Pia imedaiwa Zuchu na Diamond walishaachana muda kidogo kabla ya sherehe ya mama Diamond Platnumz, Bi Sandra, kisa usaliti wa Diamond, na ndiyo maana siku ya tukio la sherehe diamond alikuwa anajiachia sana na ma ex bila hata kuhofia kama ana mke.

ZUCH 05

Safari iliyoanza kwa tetesi
Zuchu alijiunga na WCB Wasafi mwaka 2020, hatua iliyomfanya kuwa msanii wa pili wa kike kusajiliwa chini ya lebo hiyo.

Muda mfupi baadaye zilianza tetesi za ukaribu wake na Diamond Platnumz. Ingawa kwa muda mrefu walikanusha kuwa wapenzi, picha, video na safari walizokuwa wakifanya pamoja ziliendelea kuwafanya mashabiki kuamini kulikuwa na zaidi ya uhusiano wa kikazi.

Baada ya miezi kadhaa ya mjadala, wawili hao baadaye waliweka wazi walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi, jambo lililowafurahisha mashabiki wao huku likiwaacha wengine wakisubiri kuona kama safari hiyo ingeishia kwenye ndoa.

ZUCHU

Penzi lililotawaliwa na misukosuko
Licha ya kuonekana kuwa mmoja wa wanandoa maarufu kwenye tasnia ya burudani Afrika Mashariki, uhusiano wa Diamond na Zuchu haukukosa misukosuko.

Katika nyakati tofauti tangu walipoweka wazi mahusiano yao, wawili hao waliwahi kuhusishwa na taarifa za kuachana na baadaye kurudiana.

Mwaka 2024, Diamond aliwahi kuandika kwenye mitandao ya kijamii alikuwa "single", jambo lililozua mjadala mkubwa kabla ya baadaye kufafanua kauli yake.

Miezi kadhaa baadaye, Zuchu naye aliwahi kutangaza walikuwa wameachana, lakini baada ya muda walionekana tena wakiwa pamoja na kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Matukio hayo yaliwafanya mashabiki wengi kuamini wawili hao walikuwa wakipitia vipindi vya migogoro ambavyo mara nyingi vilimalizika kwa maridhiano.

ZUCH 04

Kauli za Zuchu zilizowahi kuzua mjadala
Katika kipindi chote cha uhusiano wao, Zuchu aliwahi kuchapisha jumbe mbalimbali Instagram na kuzungumzia changamoto za mahusiano katika mahojiano tofauti.

Baadhi ya jumbe zake zilitafsiriwa na mashabiki zilikuwa zikielezea maumivu aliyokuwa akiyapitia ndani ya uhusiano wao. Wakati mwingine aliandika akidokeza alikuwa akiumizwa na mambo yaliyokuwa yakitokea kwenye maisha yake ya kimapenzi, huku mashabiki wengi wakihusisha kauli hizo na madai ya usaliti.

Kwa upande wake, Diamond aliendelea kusisitiza mara kadhaa changamoto za kimapenzi ni jambo la kawaida na hakuwahi kuthibitisha madai hayo.

ZUCH 03

Ndoa iliyowapa matumaini mashabiki
Baada ya miaka kadhaa ya mahusiano yenye kupanda na kushuka, Diamond na Zuchu walithibitisha walikuwa wamefunga ndoa ya Kiislamu.

Habari hiyo iliwapa matumaini mashabiki wengi waliokuwa wakiamini kuwa migogoro yote ilikuwa imebaki historia na wawili hao wangeanza ukurasa mpya wa maisha.

Katika kipindi hicho walionekana mara kadhaa wakishirikiana kwenye shughuli za kifamilia na kikazi, hali iliyowafanya wengi kuamini ndoa yao ilikuwa imara.

ZUCH 02

Sherehe ya Mama Dangote yazua mjadala
Siku chache kabla ya Zuchu kutangaza talaka, mitandao ya kijamii ilijaa mijadala iliyohusu sherehe ya kutimiza miaka 59 ya Mama Dangote.

Mwanaspoti lilihudhuria sherehe hiyo na kushuhudia baadhi ya matukio yaliyozua mjadala mkubwa mtandaoni.

Kabla ya sherehe hiyo, video zilizosambaa zilimuonyesha mtangazaji Aliya akimpelekea Mama Dangote keki nyumbani kwake Madale. Video hizo zilichochea maoni mengi kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, huku baadhi wakitoa tafsiri zao kuhusu uhusiano wa familia hiyo.

Aidha, kwenye sherehe hiyo walionekana pia baadhi ya wanawake waliowahi kuhusishwa kimapenzi na Diamond Platnumz, jambo lililoendelea kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, hakuna ushahidi unaoonyesha matukio hayo ndiyo yaliyosababisha kuvunjika kwa ndoa ya Diamond na Zuchu.


Mwisho wa safari ya miaka sita
Kwa sasa, kauli ya Zuchu imeweka rasmi mwisho wa safari ya miaka sita ya uhusiano uliopitia vipindi vya furaha, mafanikio, migogoro, kuachana, kurudiana na hatimaye ndoa.

Iwapo wawili hao watakamilisha mchakato wa talaka, itakuwa mwisho wa moja ya mahusiano yaliyovuta hisia za mashabiki wengi wa muziki Afrika Mashariki kwa miaka kadhaa.

Kwa sasa, macho ya mashabiki yameelekezwa kwa Diamond Platnumz kusubiri kama atatoa kauli yake kuhusu tangazo la Zuchu au ataendelea kubaki kimya kama alivyofanya katika baadhi ya migogoro iliyopita. Na tufahamu Zuchu kwa sasa ni mjamzito wa kujifungua muda wowote kuanzia sasa.