Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tamasha la Pasaka kufanyika Leaders, hakuna kiingilio

Katika kuungana na watanzania kuadhimisha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan Suluhu waandaaji wa tamasha la Pasaka wameondoa kiingilio kwa watu watakaokwenda kwenye tamasha hilo.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Machi 19, 2023 na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama ambao ndio waandaji wa tamasha hilo linalitarajia kufanyika Aprili 9, 2023.


Msama  amesema tamasha hilo ambalo litafayika viwanja vya Leaders wameamua kulifanya bure ili watanzania wengi zaidi  wajumuike katika kusherekea miaka miwili ya Rais Samia.


"Rais katufanyia watanzania mambo mengi na mazuri katika kipindi chake cha miaka miwili hivyo tumeona tulitumie tamasha hili kusheherekea naye pamoja na watanzania kwa ujumla mafanikio yake hayo kwenye tamasha la mwaka huu" amesema Msama.


Mkurugenzi huyo amesema tayari wasanii mbalimbli wameshathibitisha uwepo wao akiwemo John Lisu, Upendo Nkone  Zablon Sing'er, Jesca BM, Beatrice Mwaipaja, Ambwene Mwaisonge, Tumaini Akilimali na Faustine Munishi kutoka nchini Kenya.
Kwa upande wake Mwakilishi wa kwaya ya Zablon Sing'er, Emmanuel Zablon aliwaomba watu siku hiyo kujitokeza kwa wingi kwa kuwa wamewaandalia mambo mazuri ikiwemo kuwa wa kwanza kusikiliza nyimbo zao mpya.


Naye Upendo Nkone amesema hiyo siku ni mtoko wakueleweka hivyo watu hawapaswi kukosa na kuahidi kuwapa watu burudani kwa njia ya kumtukuza Mungu.