Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harmonize ndani ya Serengeti Festival leo, Mchengerwa ataka wasanii kuitangaza Tz

Tamasha la Muziki la Serengeti leo Machi 13, 2022 linaingia katika siku yake ya pili na ya mwisho katika viwanja wa Chinangali jijini Dodoma baada ya kazi nzuri ya jana huku msanii Harmonize kuwa miongoni mwa wasanii wataopanda jukwaani.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewataka wasanii waliopata fursa kushiriki katika tamasha hili kutoa burudani kabambe ili kuonyesha vipaji vyao na kuitangaza Tanzania.

Wasanii waliopanda jana waliwapagawisha mamia ya  wapenzi waliofurika kuwaburudisha kutokana na umahiri wao wa kutumbuiza, huku wengine wakifanya kolabo kama AY na  Mbunge wa Muheza na Msanii Mkongwe Mwana FA na kuwa miongoni mwa vivutio katika tamasha hili.

Kundi la wasanii machachali na chipukizi wataungana na wakongwe  ambao watahitimisha tamasha la mwaka huu leo Machi 13, 2022 kwa kiingilio cha  Sh 3,000 getini.

Mbali na wasanii wengi watakao burudisha leo Ma Dj wakongwe wanatarajia kutawala jukwaa kwa vionjo vyao.

Kutokana na uratibu nzuri wa tamasha hili ambalo limeratibiwa na Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana  na wadau kumekuwa na shauku kubwa kwa Wasanii mbalimbali kufanya vizuri ili waweze kuinua  viwango vyao.

Jana wakati wasanii wakitumbuiza Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitoa msimamo wa kuendelea kuandaa na kuboresha tamasha ili kuendelea kutumia sanaa kuitangaza Tanzania kimataifa.