Yanga yasukwa upya KOCHA wa Yanga, Sam Timbe amebadili staili na mfumo wa timu hiyo na amewapa mbinu mpya mastraika wake saba huku akiwasha moto mpya na sasa mashambulizi yote yataanza kwa mabeki wa pembeni, Shadrack...
Simba yaua, Yanga mdebwedo MABINGWA wa Ngao ya Jamii, Simba wameendeleza makali yao kwa kuichapa JKT Oljoro 2-0 katika mchezo ulioshuhudia kadi nyekundu mbili, huku mabingwa watetezi Yanga wakipokea kichapo cha bao 1-0...
Brazil yatwaa ubingwa wa Dunia U20 MSHAMBULIAJI Oscar alifunga mabao matatu na kuisaidia Brazil kushinda 3-2 dhidi Ureno kwenye muda wa nyongeza wakati wa fainali za Kombe la Dunia kwa vijana U-20 p.
Brazil, Misri, Argentina zakaa pazuri TIMU ya Brazil ilichapa Austria 3-0, huku Argentina wakilazimishwa suluhu na watani zao England kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya miaka 20 yanayoendelea nchini Colombia.
Timbe aingia na gia mpya Yanga KOCHA Sam Timbe haishi mambo. Sasa ametua Yanga na gia mpya ambayo amemkabidhi fowadi wake Mghana Kenneth Asamoah na kufanya siri kubwa huku akiwapiga wachezaji mchakamchaka kila asubuhi.
First eleven mpya Yanga, Simba kiboko USAJILI wa Yanga na Simba sasa unaleta raha. Vikosi vilivyosajiliwa na timu hizo unaweza kutengeneza vikosi viwili kila moja na kucheza kwa fomesheni yoyote ile kutokana na uwezo, uzoefu na ujuzi...
Yanga yaipiga bao jingine Simba SC SAHAU bao la Kenneth Asamoah. Yanga imeipiga bao jingine Simba katika takwimu za mchezo wa fainali wa Kombe la Kagame.
Hii ndo Yanga bana yalipa kisasi cha miaka 20 KENNETH Asamoah amethibitisha kwamba yeye ni profesheno. Bao lake safi la videoni dakika ya 108 limeipa Yanga Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuwanyamazisha kabisa...
Fabregas asaini miaka miwili Yanga HARUNA Niyonzima 'Fabregas' wa Rwanda amesaini mkataba wa miaka miwili kuchezea Yanga, lakini APR imesisitiza kuwa kiungo huyo hauzwi.
Congo United yaongoza kwa usajili CONGO United ya Mombasa ndiyo klabu inayoongoza kwa kutema na kusajili wanasoka wengi nchini Kenya.