Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaipiga bao jingine Simba SC

Nahodha wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa Mwandemele akiwaongoza wachezaji wenzake kusherehekea ubingwa wa mashindano ya Kagame

CALVIN KIWIA SAHAU bao la Kenneth Asamoah. Yanga imeipiga bao jingine Simba katika takwimu za mchezo wa fainali wa Kombe la Kagame. Mchezo huo uliochezwa kwa dakika 120 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi Jumapili, Yanga ilipata bao dakika ya 108 lililofungwa na Kenneth Asamoah kwa kichwa akiunganisha krosi ya Rashid Gumbo aliyetokea benchi akichukua nafasi ya Juma Seif 'Kijiko' aliyeumia. Pasi 524 zilichezwa kwenye pambano hilo kutoka kwa wachezaji 28 wa timu zote mbili ikiwa ni pamoja na wale waliotokea benchi. Pasi hizo ni sawa na wastani wa pasi 18 kwa kila mchezaji. Mabingwa wapya wa Kombe la Kagame, Yanga waliwazidi kete Simba kwa kucheza pasi 307, sahihi zikiwa 266 huku 41 zikienda fyongo. Simba walipiga pasi 217, sahihi zikiwa 154 na 63 zikipotea njia, lakini huenda kuumia kwa kiungo wao, Mwinyi Kazimoto dakika ya 17 kuliwaathiri vijana wa Msimbazi. Fundi wa kupiga pasi kwenye mpambano huo alikuwa kiungo wa Yanga, Juma Seif 'Kijiko' aliyecheza pasi 49. Kati ya hizo 38 ziliwafikia walengwa na 11 zikienda fyongo hata hivyo hakumaliza mchezo huo baada ya kuumia dakika ya 63. Patrick Mafisango wa Simba alicheza pasi 35, sahihi 19 na 16 fyongo. Tatizo kubwa la Mafisango ilikuwa ni kugeuka nyuma kila alipopata mpira na kupiga pasi bila kutazama anayempigia. Simba iliibuka kinara wa kutoa mipira nje ya uwanja baada ya kufanya hivyo mara 53 dhidi ya 44 za Yanga. Kinara wa kutoa mipira nje alikuwa beki mpya wa Simba, Said Nassor 'Cholo' aliyetoa mara 16 kwa nia ya kutibua mipango ya washambuliaji wa Yanga, Davies Mwape, Hamis Kiiza na Jerryson Tegete. Yanga walilifikia lango la watani wao mara 12 na kupiga mashuti saba manne yakienda nje ya lango na matatu kupanguliwa na Juma Kaseja na kupata kona saba. Simba walilifikia lango la Yanga mara 11 na kupiga mashuti nane, matano yakitoka nje na matatu yakinyakwa na Yaw Berko na kupata kona tano. Mwamuzi wa pambano hilo Wiish Yabarow kutoka Somalia aliwaonyesha kadi za njano Oscar Joshua na Yaw Berko wa Yanga kwa kuchelewesha muda na Salum Kanoni wa Simba. Kabla ya kutoka Mwinyi Kazimoto, Simba ilionekana kuukamata mchezo, lakini kuingia kwa Mohammed Banka kuliimaliza zaidi Simba kwani alitumia muda mwingi kucheza na vivuli vya wachezaji wa Yanga. Pia kutolewa kwa Shija Mkina ambaye alikuwa na nguvu nyingi pamoja na kukaba na kuingia kwa Salum Machaku kuliifanya sehemu ya kiungo ya Simba kufa na kuwafanya Rashid Gumbo na wenzake kutawala zaidi.