Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yasukwa upya

Kikosi cha Yanga

MICHAEL MOMBURI KOCHA wa Yanga, Sam Timbe amebadili staili na mfumo wa timu hiyo na amewapa mbinu mpya mastraika wake saba huku akiwasha moto mpya na sasa mashambulizi yote yataanza kwa mabeki wa pembeni, Shadrack Nsajigwa na Oscar Joshua. Lakini Timbe ambaye aliipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Kagame ndani ya miezi sita amesita kuwapa mastraika hao masharti kama ya Wayne Rooney wa Man United na Didier Drogba wa Chelsea. Hata hivyo, mastraika kama Kigi Makassy, Pius Kisambale, Hamis Kiiza, Davies Mwape, Kenneth Asamoah, Jerry Tegete na Julius Mrope wataibuka katika mechi dhidi ya Mtibwa, Septemba 7. Katika mazoezi ya saa tatu jana Ijumaa asubuhi kwenye Uwanja wa Kaunda jijini Dar es Salaam, kocha huyo alikuwa akiwaamuru wachezaji mambo yafuatayo, kugusa mpira mara moja tu (one touch), kucheza na kufanya uamuzi wa haraka, pasi fupi fupi na kutoruhusu mpira kudunda chini. Mambo mengine aliyokuwa akisisitiza kocha huyo ni wachezaji kufungua uwanja na kucheza mpira pembeni. Katika staili yake mpya, mashambulizi yote yataanzia kwa mabeki wa pembeni ambao jana Ijumaa walikuwa Godfrey Taita na Abuu Ubwa na si kipa au mchezaji mwingine. Mabeki hao wanapaswa kupiga moja kwa moja kwa mastraika kisha mpira urudi kwenye kiungo ndipo usogezwe kwa mawinga wa pembeni wapige krosi na vitendo hivyo kila kimoja si zaidi ya sekunde jambo ambalo lilifanya wachezaji wengi kutoka jasho na kuwa hoi kupindukia ingawa baadhi walikuwa wakishindwa kuhimili. Baada ya mazoezi, Timbe aliiambia Mwanaspoti kuwa; "Nimeamua kubadili staili na sasa timu itakuwa ikishambulia kutokea pembeni kutokana na jinsi Uwanja wa Morogoro ulivyo, inakuwa ngumu sana kufanikiwa kwa kutumia washambuliaji wawili wa pale mbele." Hiyo ina maana kuwa mashambulizi yote ya Yanga yataanzia kwa Oscar au Nsajigwa na mipira kuelekezwa kwa Mwape na Asamoah au Tegete na baadaye kurudishwa kwa viungo ambao watawakabidhi mawinga ambao watakapoinasa tu tayari mastraika wote watakuwa kwenye boksi. "Haina maana kwamba kila siku nitatumia staili hiyo lakini najua jinsi ya kucheza nayo kiufundi zaidi kukabiliana na hizi timu ninazocheza nazo. Kuhusu malengo siwezi kuwapa washambuliaji wangu kiwango cha magoli ya kufunga, nitakuwa nimewapa mzigo sana. "Nikimpa kwa mfano Mwape, Asamoah au Tegete kwamba anifungie magoli 20 au zaidi msimu huu nitamweka kwenye presha kubwa sana na hata umakini wake utapungua kwavile kila mara atakuwa anafikiria tu kutimiza malengo na hata kuharibu akili yake na kumfanya kutoka mchezoni kabisa. "Ukiangalia wachezaji kama Rooney au Drogba bado hawajatisha kwenye msimu mpya kwavile wana malengo makubwa na wanataka kushinda zaidi ili kuvuka zile rekodi zao za msimu uliokwisha, lakini kama wangekuwa huru isingekuwa hivyo. Ninachotaka mimi Yanga ishinde kwa idadi yoyote ya magoli halafu mambo mengine yatafuata. Haijalishi nani atafunga na anacheza nafasi gani. Huo ndio msimamo wangu na wachezaji wanajua ndio maana wako kitimu zaidi,"alisisitiza Timbe.