Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Brazil yatwaa ubingwa wa Dunia U20

Kiungo wa Brazil, Philippe Coutinho (katikati) akijaribu kuwatoka wachezaji wa Ureno, Pele (mbele) na beki Mario Rui wakati wa fainali za Kombe la Dunia kwa vijana U-20 machi iliyofanyika jijini Bogota. Brazil ilishinda 3-2. Picha na APF

BOGOTA, Colombia MSHAMBULIAJI Oscar alifunga mabao matatu na kuisaidia Brazil kushinda 3-2 dhidi Ureno kwenye muda wa nyongeza wakati wa fainali za Kombe la Dunia kwa vijana U-20 p. Oscar alifunga bao la ushindi dakika 111, kwa kupiga shuti la mguu wa kulia lililompita kipa wa Ureno, Mika. Chipukizi huyo wa Brazil alifunga bao la dakika 5 na 78. Alex alisawazisha dakika 9 kabla ya Ureno kuongoza kwa bao la Nelson Oliveira dakika 59. Brazil ilipigana kupata taji la tano la U-20, baada ya miaka miwili iliyopita kukosa ubingwa huo. Ureno ilikuwa ikisaka taji la tatu. Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Mexico ilichapa Ufaransa 3-1. Mabao ya Ulises Davila, Jorge Enriquez na Edson Rivera walizima ndoto za bao la kuongoza la Alexandre Lacazette alilolifunga kwa Ufaransa katika dakika ya 8. Kumaliza mshindi wa tatu kumetoa mwanga mwema kwa Mexico; ambayo miezi mitatu iliyopita timu yao ya wakubwa iliwafunga Marekani na kutwaa Gold Cup mwezi Juni, pia timu ya vijana ya Mexico ilitwaa Kombe la Dunia kwa vijana wa U-17 mwezi Julai.