AC Milan yamaliza kwa Mateta, Glasner achelewesha MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace, Jean-Phillipe Mateta amefanya makubaliano binafsi na AC Milan juu ya kujiunga nao kwa mkataba utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2030.
Arsenal yapata pigo tena, yampoteza Saka MBIO za ubingwa kwa Arsenal zimezidi kuingiwa na mikosi baada ya staa wao, Bukayo Saka kupata majeraha yaliyosababisha kutocheza kwenye mechi dhidi ya Leeds United na aliumia dakika za mwisho...
Nidhamu tatizo kwa Bellingham, Bruno atajwa REAL Madrid inaripotiwa kuhitaji kumsajili mmoja wa nyota wa Manchester United kama mbadala wa Jude Bellingham, kutokana na madai ya kuwepo kwa utovu wa nidhamu kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa...
Michael Carrick anamtaka Rashford Man United KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick anataka kumrejesha mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford anayecheza kwa mkopo Barcelona ikiwa atateuliwa kuwa kocha mkuu wa kudumu wa klabu hiyo.
Chelsea inataka kusajili maeneo yote CHELSEA inaendelea kutafuta wachezaji katika nafasi zote wakati dirisha la usajili likitarajiwa kumalizika usiku wa leo.
Walipa kodi mashuhuri Ligi Kuu England STAA wa Manchester City, Erling Haaland anaongoza katika orodha ya wachezaji wa Ligi Kuu England waliolipa kodi kubwa zaidi, takribani Pauni 16.9 milioni mwaka jana.
Arsenal yarudisha makali, yaichapa Leeds kwao ARSENAL imekomesha mfululizo wa mechi tatu bila ushindi kwenye Ligi Kuu England baada ya kuibabua Leeds United mabao 4-0 katika Uwanja wa Elland Road, Jumamosi.
Arne Slot akubali kukosolewa KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, anakiri kuwa ni haki kupuuzia mafanikio ya msimu uliopita na kumhukumu yeye binafsi kwa misingi ya msimu wa sasa pekee, huku presha ikizidi kumkabili Mdachi huyo...
Declan Rice ajiweka anga za wababe England DECLAN Rice amekuwa mchezaji wa tano Mwingereza kwa umri mdogo zaidi katika historia ya Ligi Kuu England kufikisha mechi 300.
Carrick afunguka ishu ya Fernandes KOCHA wa muda wa Manchester United, Michael Carrick anasisitiza kuwa watasubiri hadi Juni mwaka huu ili kuamua mustakabali wa nahodha wao, Bruno Fernandes.