Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chelsea inataka kusajili maeneo yote

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Kipaumbele kikubwa kwa Chelsea hivi sasa ni kusajili beki wa kati na mazungumzo yanaendelea na Rennes kwa ajili ya Jeremy Jacquet.

LONDON, ENGLAND: CHELSEA inaendelea kutafuta wachezaji katika nafasi zote wakati dirisha la usajili likitarajiwa kumalizika usiku wa leo.

Kipaumbele kikubwa kwa Chelsea hivi sasa ni kusajili beki wa kati na mazungumzo yanaendelea na Rennes kwa ajili ya Jeremy Jacquet.

Lakini mbali ya fundi huyo, kocha Liam Rosenior amesisitiza bado anahitaji kuboresha baadhi ya maeneo katika kikosi hicho.

"Kila eneo ninalitazama ili kuongeza nguvu. Kazi yangu katika soko la usajili, kwa kushirikiana na wenzangu, ni kuhakikisha kikosi kinakuwa imara iwezekanavyo katika kila idara. Iwe ni winga, mshambuliaji au beki. Tukiona mchezaji najua wenzangu wako tayari kuhakikisha tunampata kuhakikisha anasajiliwa na anaiboresha timu. Sitaki kusajili wachezaji kwa sababu nimeamua tu, nataka kuleta wachezaji ambao wanakuja kuongeza kitu."

Hata hivyo, Chelsea huenda wakawa na shughuli nyingi zaidi upande wa wachezaji wanaoondoka kuliko wale wanaoingia.

Rosenior hataki kumpoteza mshambuliaji Marc Guiu wala beki Josh Acheampong, lakini aliacha mlango wazi kwa Tyrique George kuondoka.

Aidha, matajiri hawa wanafanya kazi ya kumtafutia timu Axel Disasi, ambaye alirejea mazoezini baada ya kuondolewa kikosi cha kwanza kwa muda na Enzo Maresca.