Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yapata pigo tena, yampoteza Saka

SAKA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akitarajiwa kuanza upande wa kulia wa safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.

LONDON, ENGLAND: MBIO za ubingwa kwa Arsenal zimezidi kuingiwa na mikosi baada ya staa wao, Bukayo Saka kupata majeraha yaliyosababisha kutocheza kwenye mechi dhidi ya Leeds United na aliumia dakika za mwisho kabla ya mechi kuanza.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alikuwa akitarajiwa kuanza upande wa kulia wa safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.

Hata hivyo, Saka alionekana kuondoka ghafla uwanjani na kwenda vyumbani akiwa ameongozana na mtaalamu wa tiba (physio) baada ya kuhisi maumivu.

Arsenal ilithibitisha Noni Madueke ndiye aliyechukua nafasi yake baada ya wataalam wa afya kuthibitisha hawezi kuendelea.

Kengele za hatari zilianza kulia kwa mashabiki wa Arsenal pale Saka aliposhindwa kurejea uwanjani baada ya kuelekea moja kwa moja chumba cha kubadilishia nguo.

Baadaye, kocha wa mazoezi ya viungo Sam Wilson alionekana akimfanyia Madueke mazoezi ya ziada, ili achukue nafasi ya fundi huyo.

Kuumia kwa Saka ambaye inadaiwa alipata shida kwenye nyonga (hip), kulimfanya Christian Norgaard kuwekwa benchi baada ya kusafiri kwenda Leeds kama mchezaji wa ziada asiyekuwepo benchi.

Kikosi cha Mikel Arteta kilikuwa kinataka kushinda mechi hiyo ili kupunguza pengo la alama kati yao ya wapinzani wao Manchester City ambao jana walicheza dhidi ya Tottenham.

Hata hivyo, Arsenal wanatumaini jeraha la Saka halitomuweka nje kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England amefunga mabao saba na kutoa pasi saba za mabao katika mechi 31 msimu huu.

Hii inakuwa ni mara ya pili Saka kuumia, mwanzoni mwa msimu huu alikosa baadhi ya mechi muhimu kutokana na jeraha la misuli ya paja.

Moja kati ya mechi muhimu ambazo Arsenal inatamani Saka arudi ili acheze ni ile ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Chelsea.

Arsenal inaingia kwenye mechi hiyo ya Jumanne katika uwanja wa Emirates ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 3-2 ilioupata katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

Licha ya kumkosa Saka katika mechi hiyo dhidi ya Leeds, Arsenal bado iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.