Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Declan Rice ajiweka anga za wababe England

Muktasari:

  • Kiungo huyo ghali wa Arsenal alitazamiwa kuweka rekodi uwanjani Elland Road, Jumamosi wakati kikosi cha The Gunners kilipomenyana na Leeds United katika mchezo muhimu wa mikikimikiki hiyo ya ligi.

LONDON, ENGLAND: DECLAN Rice amekuwa mchezaji wa tano Mwingereza kwa umri mdogo zaidi katika historia ya Ligi Kuu England kufikisha mechi 300.

Kiungo huyo ghali wa Arsenal alitazamiwa kuweka rekodi uwanjani Elland Road, Jumamosi wakati kikosi cha The Gunners kilipomenyana na Leeds United katika mchezo muhimu wa mikikimikiki hiyo ya ligi.

Arsenal ilihitaji ushindi wa kila aina katika mchezo huo ili kujiondoa kwenye presha kubwa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Hivyo basi, kiungo huyo wa timu ya taifa ya England alikuwa na jukumu kubwa la kutimiza. Rice ni nahodha wa Arsenal, hata kama havai beji ya unahodha.

Nahodha rasmi ni Martin Odegaard, lakini licha ya kushinda kura ya wachezaji msimu uliopita kuendelea na jukumu hilo, bado haonekani kuwa kiongozi wa asili. Kutokana na kiwango chake duni tangu arejee kutoka kwenye majeraha, Odegaard amekuwa akigonganisha mawazo ya wengi kuhusu hatima yake katika kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta.

Na sasa Rice, anapewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha wa Arsenal na pia timu ya taifa ya England kwa siku zijazo. Akiwa na umri wa miaka 27 na siku 17, Rice Jumamosi alitarajia kufikisha mechi 300 kwa kasi zaidi kuliko waliokuwa viungo wa England, Frank Lampard na Steven Gerrard. Tayari, Rice anaweza kutajwa sambamba na wachezaji hao wakubwa, na anatarajia kufanikisha makubwa kwa klabu na taifa.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alikiri: “Nimekuwa nikisema mara zote kwamba sijui mipaka ya Declan iko wapi. Kadri unavyokaa naye zaidi, kumuangalia mazoezini na kwenye mechi, ndivyo anavyozidi kuwa bora. Kwa nini? Kwa sababu hamu yake ya kuendelea kuboresha kiwango ipo muda wote. Ana uthabiti wa hali ya juu. Kimwili ni bora sana, na kiakili ni mchezaji anayemudu kila aina ya presha.”