Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AC Milan yamaliza kwa Mateta, Glasner achelewesha

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kila kitu kinaonekana kuwa katika mstari na klabu zote mbili zimeshafanya makubaliano lakini changamoto kubwa inaonekana kwa Kocha wa Palace, Oliver Glasner ambaye anadaiwa kuwaambia mabosi wa timu hiyo hatamruhusu Mateta mwenye umri wa miaka 28, kuondoka wapate mbadala wake.

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace, Jean-Phillipe Mateta amefanya makubaliano binafsi na AC Milan juu ya kujiunga nao kwa mkataba utakaomfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwaka 2030.

Kila kitu kinaonekana kuwa katika mstari na klabu zote mbili zimeshafanya makubaliano lakini changamoto kubwa inaonekana kwa Kocha wa Palace, Oliver Glasner ambaye anadaiwa kuwaambia mabosi wa timu hiyo hatamruhusu Mateta mwenye umri wa miaka 28, kuondoka wapate mbadala wake.

Mateta anasubiri ruhusa ya kusafiri Italia kwa ajili ya  vipimo vya afya, lakini uamuzi wa mwisho kuhusu dili hilo uko mikononi mwa Crystal Palace, hususan kwa Glasner ambaye kwa sasa anatafuta mshambuliaji.

Palace imetoka kuuza mchezaji wake tegemeo Marc Guehi hivi karibuni jambo ambalo kocha Glasner lilionekana kumkera sana kiasi cha kuripotiwa anataka kujizulu.

Hadi sasa haijapata mbadala wake na hiyo inamfanya  Glasner kutohitaji Mateta naye aondoke kabla hajapata majeraha.

Mkataba wa sasa wa Mateta unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao 10.


Joe Willock

FULHAM imeshindwa kufanikisha usajili wa kiungo wa Newcastle United raia wa England, Joe Willock, 26, baada ya ofa yao ya Pauni 20 milioni kukataliwa.

Newcastle imesisitiza haitaruhusu Willock kuondoka hadi itakapopata mbadala wake wa kudumu katika safu ya kiungo. Willock amekuwa akionyesha kiwango cha juu.

Kwa sasa Fulham inafanya mazungumzo zaidi ikiwezekana itume ofa mpya katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu.


Mohamed Kader Meite

CHELSEA na Manchester United zinafuatilia kwa karibu mshambuliaji chipukizi wa Rennes na Ufaransa, Mohamed Kader Meite, 18.

Klabu hizo zilituma maskauti wake kwenda kumtazama Meite akicheza mara kadhaa katika Ligi Kuu Ufaransa na ripoti zinaonyesha wamevutiwa naye sana.

Rennes inamwona kama mchezaji muhimu katika mipango yao hivyo inahitaji ofa nono inayoweza kufikia Pauni 40 milioni ili kumuuza.


Tyrique George

SUNDERLAND na Everton zimeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya vijana ya England, Tyrique George, 19.

George anawindwa pia na timu mbalimbali kutoka Hispania, Ufaransa na Italia, kutokana na kiwango chake na uwezo wa kufunga mabao.

Chelsea ipo tayari kumtoa kwa mkopo  kuhakikisha mchezaji huyo anaendelea kukua bila kwa kupata muda mwingi wa kucheza.


Jhon Duran

TOTTENHAM Hotspur na Leeds United ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu England zilizopatiwa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Jhon Duran, 22, ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Fenerbahce akitokea Al-Nassr.

Duran amekuwa na wakati mzuri Fenerbahce tangu ajiunge nao dirisha lililopita la majira ya kiangazi, jambo lililomfanya kuingia kwenye rada ya klabu kadhaa kubwa Ulaya. Klabu hizo ziko tayari kuwasilisha ofa.


Jeremy Jacquet

LIVERPOOL na Chelsea zipo katika mazungumzo na Rennes kwa ajili ya kumsajili beki wa klabu hiyo, Mfaransa, Jeremy Jacquet, 20. Hata hivyo, Jacquet ataweza kuhamia England dirisha lijalo la majira ya kiangazi na sio kwa sasa.

Jacquet ni miongoni mwa mastaa chipukizi wenye vipaji walioonekana Ligue 1 kwa msimu huu na Rennes haitaki kumwachia kwa sasa, kwa sababu itakuwa ngumu kusajili mbadala wake.


Mamadou Sarr

CHELSEA inataka kumrejesha beki wao, Mamadou Sarr, 20, kutoka Strasbourg ambako kwa sasa anacheza kwa mkopo msimu mmoja.

Sarr amekuwa akionyesha maendeleo makubwa Ligue 1 kiasi cha kuwavutia Chelsea wanaoamini akirudi atasaidia sana timu.

Vilevile inaelezwa benchi la ufundi la Chelsea ambalo ndilo lilikuwa likihudumu Strasbourg linamhusudu sana staa huyo.


David Datro Fofana

AUXERRE inataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, David Datro Fofana, 23.

Fofana amekuwa hapati nafasi ya kutosha kikosi cha kwanza cha Chelsea na mabosi wa timu hiyo wapo tayari aidha kumuuza au kumtoa kwa mkopo  ili apate muda mwingi zaidi wa kucheza mara kwa mara.

Auxerre inataka kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ushambuliaji kabla ya dirisha hili la majira ya baridi kufungwa.