Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carrick afunguka ishu ya Fernandes

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa Kireno anatafakari hatua yake inayofuata na anatarajiwa kupokea ofa nyingi kutoka kwa klabu mbalimbali mwishoni mwa msimu.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa muda wa Manchester United, Michael Carrick anasisitiza kuwa watasubiri hadi Juni mwaka huu ili kuamua mustakabali wa nahodha wao, Bruno Fernandes.

Kiungo huyo wa Kireno anatafakari hatua yake inayofuata na anatarajiwa kupokea ofa nyingi kutoka kwa klabu mbalimbali mwishoni mwa msimu.

Fernandes ameanza kukata tamaa kutokana na namna klabu inavyoendeshwa pamoja na mabadiliko ya mara kwa mara ya benchi la ufundi. Alikuwa karibu kuondoka Man United wakati wa dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini alikataa nafasi ya kujiunga na miamba ya Saudi Pro League.

Ingawa Fernandes amevutiwa na mchango ambao Carrick ameutoa kama kocha wa muda, bado anataka kuona ni nani atakayeteuliwa kuwa kocha wa kudumu na kama Man United watafanikiwa kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anafahamu kuwa mkataba wake ujao utakuwa mkubwa wa mwisho katika taaluma yake, na anahitaji kuhakikisha anapata malipo makubwa. Man United italazimika kumpa Fernandes mkataba mpya ulioboreshwa wa takribani Pauni 400,000 kwa wiki ili kuwa na nafasi ya kumbakiza. Mkataba wake wa sasa unaendelea hadi Juni 2027, lakini una kipengele cha kununuliwa kwa Pauni 60 milioni.

Carrick anasisitiza kuwa kwa sasa Fernandes bado ana furaha na ana dhamira kamili ya kuitumikia Man United, lakini mazungumzo kuhusu mustakabali wake yatafanyika kuelekea mwisho wa msimu.

Alisema: “Sote tunataka kushinda mataji. Sote tunataka kuwa bora zaidi. Tunataka kuendelea kuboresha kama timu. Tunataka kufanikiwa na hilo ni jambo tunalopaswa kulifanyia kazi kwa pamoja, lakini Bruno amekuwa mzuri sana tangu nifike hapa. Alikuwa mzuri pia nilipokuwa hapa awali, kwa hiyo sina lolote baya la kusema kumhusu. Hilo si jambo la kukimbilia sana, unajua. Mustakabali wake uko kwenye ajenda kwa kiasi fulani, lakini ajenda yangu kuu kwa sasa ni kuumaliza vizuri mchezo wa Jumapili dhidi ya Fulham. Bruno amejitolea kikamilifu. Hakuna tatizo lolote kabisa kwa upande huo. Mambo ya baadaye yatajadiliwa kuelekea mwisho wa msimu au wakati unaofaa. Kwa sasa kila kitu ni chanya.”