Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michael Carrick anamtaka Rashford Man United

CARRICK Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo, ameiongoza Man United katika mechi mbili pekee, lakini tayari amepata ushindi mkubwa dhidi ya Manchester City na Arsenal.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick anataka kumrejesha mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford anayecheza kwa mkopo Barcelona ikiwa atateuliwa kuwa kocha mkuu wa kudumu wa klabu hiyo.

Carrick ameanza vyema kipindi chake kama kocha wa muda, baada ya kuchukua nafasi ya Ruben Amorim aliyefutwa kazi.

Kiungo huyo wa zamani wa timu hiyo, ameiongoza Man United katika mechi mbili pekee, lakini tayari amepata ushindi mkubwa dhidi ya Manchester City na Arsenal.

Mwanzo huo mzuri umeibua tetesi Carrick anaweza kupewa nafasi ya ukocha wa kudumu mwishoni mwa msimu na inaelezwa ikiwa hilo litatokea, gazeti la Telegraph limeripoti angependa kumrudisha Rashford tena Old Trafford.

Rashford alitolewa kikosini na Amorim, ambaye aliwahi kusema angependelea kumtumia kocha wa makipa mwenye umri wa miaka 63 kuliko kumchezesha mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Rashford aliichezea Aston Villa kwa mkopo mwishoni mwa msimu wa 2024/25, kabla ya kujiunga na Barcelona kwa msimu huu.

Mabingwa hao wa La Liga wana kipengele cha kumsajili moja kwa moja kwa ada ya Pauni 26 milioni na dalili zinaonyesha watakitumia kipengele hicho.

Hata hivyo, Carrick, ambaye aliwahi kucheza na Rashford katika miaka ya mwisho ya maisha yake ya soka Man United, bado anaamini kuna nafasi yake katika kikosi hicho.

Licha ya kutamani kumrudisha, ripoti nyingine zinadai Rashford mwenyewe angependa kubaki Barcelona, ambako hadi sasa amefunga mabao tisa na kutoa pasi za mabao 12.

Akizungumza baada ya kufunga bao lake katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Rashford alikiri mtindo wa uchezaji chini ya kocha Hansi Flick amechukua muda kuuzoea.

"Nadhani kwa wachezaji wa mbele tunatakiwa kuweka presha kubwa kwa mpira kadri inavyowezekana, kwa sababu tatizo linakuja pale wapinzani wanapopata muda wa kupiga pasi na kuangalia safu yetu ya ulinzi.”

Kocha Flick amekuwa akimsifu Rashford mara kwa mara na kudokeza uamuzi wa mwisho kuhusu mustakabali wake utakuwa mikononi mwa Mkurugenzi wa Michezo, Deco.