Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nidhamu tatizo kwa Bellingham, Bruno atajwa

BELLINGHAM Pict

Muktasari:

  • Tangu ajiunge na Madrid akitokea Borussia Dortmund mwaka 2023, Bellingham ameonyesha kiwango bora na amekuwa mhimili muhimu katika safu ya kiungo ya timu hiyo.

MADRID, ENGLAND: REAL Madrid inaripotiwa kuhitaji kumsajili mmoja wa nyota wa Manchester United kama mbadala wa Jude Bellingham, kutokana na madai ya kuwepo kwa utovu wa nidhamu kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England.

Tangu ajiunge na Madrid akitokea Borussia Dortmund mwaka 2023, Bellingham ameonyesha kiwango bora na amekuwa mhimili muhimu katika safu ya kiungo ya timu hiyo.

Hata hivyo, licha ya uwezo wake, mara kadhaa tabia zake  zinaonekana kuzua maswali mengi hata kwa wachezaji wenzake.

Baada ya Madrid kufungwa 4-2 na Benfica Jumatano, Januari 28 na kushindwa kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bellingham alionekana akiwashutumu wachezaji wenzake, akisema “hawafanyi mambo ya msingi ipasavyo” licha ya kuwa “wana vipaji”.

Kabla ya mechi hiyo, chombo cha habari cha Hispania Cadena SER kiliripoti Bellingham alikuwa miongoni mwa wachezaji watano wa Real, pamoja na Arda Guler, Franco Mastantuono, Fede Valverde na Eduardo Camavinga waliokutana na Rais wa klabu, Florentino Perez mara baada ya kuondoka kwa Xabi Alonso mapema Januari.

Inadaiwa Perez alimwomba Bellingham aonyeshe uongozi na ukomavu zaidi na akawaambia wachezaji wengine matamanio yao binafsi kuhusu nafasi wanazotaka kucheza hayapaswi kuja mbele ya masilahi ya timu, baada ya Valverde na Camavinga kulalamikia kuchezeshwa nafasi ya beki wa pembeni msimu huu.

Kwa upande mwingine, kocha mkuu wa Real Madrid, Alvaro Arbeloa alimpongeza Bellingham katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi ni mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kama mtu “anayetamani kuwa kiongozi” na “mfano wa kuigwa”.

Arbeloa amesema: “Kiwango anachokionyesha mazoezini, kujituma kwake na uongozi wake… ninajivunia sana kuwa na mchezaji kama Jude Bellingham.”

Hata hivyo, baada ya hapo, ripoti kutoka chombo kingine cha Hispania, Fichajes kilidai Bruno Fernandes yupo kwenye rada za Real Madrid dirisha la usajili wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa, hasa ikizingatiwa mkataba wa nahodha huyo wa Manchester United unaisha Juni 2027.

Ripoti hiyo inaeleza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anaweza kuvutiwa na kuhamia Madrid kwa ajili ya kupata changamoto mpya.

Fichajes pia inadai ikiwa Fernandes ataajiriwa inaweza kufungua milango kwa Bellingham kuondoka Madrid.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ureno anatajwa kuuzwa kwa takribani Pauni 43 milioni, ingawa bado haijulikani kama Man United wako tayari kumuacha staa huyo.

Kwa sasa, mkataba wa Bellingham na Madrid unamalizika mwaka 2029, huku thamani yake sokoni ikikadiriwa kuwa Pauni 100 milioni.