Kagera Sugar ina mtego wa miaka 21 WAKATI Ligi Kuu Bara ikirejea tena wikiendi hii baada ya kushuhudiwa viporo vinne vya mechi za Simba vikimalizika, Kagera Sugar ipo katika mtego wa kukwepa aibu ya miaka 21 katika ligi hiyo.
MBEYA CITY: Safari ya kushuka, kupanda ilivyogeuka pande mbili USIYEMPENDA kaja. Ndivyo unavyoweza kuelezea kurejea kwa Mbeya City ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kupotea misimu miwili, huku ikiweka rekodi na heshima jijini Mbeya.
Coastal Union yaishusha KenGold, yatangulia Championship Ken Gold imeshuka rasmi Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mchezo wake wa leo dhidi ya Coastal Union kwa mabao 2-1 uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Frii-kiki zinawavuruga JKT Tanzania KOCHA wa JKT Tanzania, Ahmad Ally, amesema ndani ya kikosi hicho kuna tatizo kwa wachezaji wake kushindwa kuzuia mashambulizi yanayotokana na mipira ya kutengwa.
Dakika 15 za kibabe Prisons ikiichezesha kwata JKT Tanzania Pamoja na kutanguliwa mabao mawili, Tanzania Prisons imetumia dakika 15 kufanya 'comeback' na kuifumua JKT Tanzania mabao 3-2 kuendeleza matumaini ya kubaki salama Ligi Kuu.
Dakika za jioooni: Tanzania Prisons presha tupu PRESHA inazidi kupanda na kushuka kwa Tanzania Prisons kutokana na matokeo iliyonayo katika Ligi Kuu Bara, huku ikitahadharishwa kutojirudia yaliyotokea msimu wa 2010/11 na 2021/22.
Chama la Wana lapiga mkwara Championship STAND United ‘Chama la Wana’ imesema dakika 90 iliyoiangalia Yanga imeona ugumu ulipo ikieleza kuwa licha ya kuiheshimu lakini haitaingia uwanjani kinyonge.
DAKIKA ZA JIOOONI: Mshale wa saa unavyoikimbiza KenGold Championship KATIKA mchezo wa soka, wanasema kosea mambo yote, lakini hakikisha timu inafanya usajili wa maana kwani ukikosea hapo tu, majuto yake ni makubwa zaidi.
Mwanjala arejea MREFA akizitaja Prisons, KenGold na Mbeya City Elias Mwanjala amerejea kukiongoza Chama Cha Soka Mbeya (MREFA) huku akizitaja Tanzania Prisons, KenGold na Mbeya City akisisitiza lazima mpira uchezwe upya.
Tanzania Prisons yamtibulia Kaseja ikiweka rekodi Sokoine Baada ya kusaka ushindi katika mechi nane mfululizo bila mafanikio, hatimaye Tanzania Prisons imeikandamiza Kagera Sugar na kumtibulia rekodi Kocha Juma Kaseja.