Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Prisons washtuka, wajipanga upya

PRISONS Pict

Muktasari:

  • Prisons inatarajia kuwa uwanjani Juni 18 kuikaribisha vinara wa Ligi Kuu na rekodi inaonyesha timu hizo zilipokutana katika mechi tano nyuma, Yanga ikishinda zote, kitu ambacho Elfadhil alisema wachezaji wa timu hiyo wanajipanga upya na benchi la ufundi ili kuisapraizi Yanga Sokoine.

WAKATI Tanzania Prisons ikijiandaa kuikabili Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, nahodha wa timu hiyo, Jumanne Elfadhil ametahadharisha wenzake kikosini kuwa tayari na historia yao na wapinzani hao ni ngumu wanapokutana uwanjani.

Prisons inatarajia kuwa uwanjani Juni 18 kuikaribisha vinara wa Ligi Kuu na rekodi inaonyesha timu hizo zilipokutana katika mechi tano nyuma, Yanga ikishinda zote, kitu ambacho Elfadhil alisema wachezaji wa timu hiyo wanajipanga upya na benchi la ufundi ili kuisapraizi Yanga Sokoine.

Hata hivyo, pamoja na unyonge huo, maafande wanajivunia mwendelezo mzuri wa matokeo katika mechi zao tatu mfululizo wakishinda dhidi ya Coastal Union 2-1, JKT Tanzania 3-2 na Ken Gold 3-1.

Hadi sasa Yanga ndiyo kinara wa ligi kwa pointi 73 wakiwania kutetea taji lao kwa msimu wan ne, huku Prisons ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi 30 ikikwepa kucheza play off.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mazoezi, Elfadhil alisema anajivunia matokeo mazuri tangu aliporejeshwa kikosini baada ya kutemwa na kupangiwa majukumu mengine nje ya uwanja.

Elfadhil alisema pamoja na mwenendo mzuri, lakini wanapokutana na Yanga huwa ni mechi ngumu, akitahadharisha wenzake kikosini kujipanga kiakili, kiushindani ili kupata pointi tatu.

“Tunajua ni mechi ngumu, Yanga ana hesabu za ubingwa sisi mipango ni kukwepa kucheza play off, tumekuwa na rekodi nzuri kwa kuwa kati ya mechi nne nyuma tumeshinda tatu na kupoteza moja. Yanga ina kikosi kikubwa na wachezaji wazuri, lazima tunapokuwa uwanjani tusipambane na mmoja, bali iwe mtu na mtu, tunaamini kila mmoja akitimiza wajibu tutashinda,” alisema Elfadhil.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Aman Josiah alisema wanachohitaji ni heshima kwa kuwa mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho Sokoine, kabla ya kumalizia msimu ugenini dhidi ya Singida Black Stars.

Alisema kwa sasa anawaandaa wachezaji kiushindani na kiakili kuhakikisha wanapokuwa uwanjani, wanapambania pointi tatu ambazo zitawaweka katika mazingira mazuri.

“Tunakutana na timu tofauti ukilinganisha na zile zilizopita, tunajiandaa kushinda na si vinginevyo, dakika 90 ndizo zitatuamulia, hii ndio mechi ya mwisho hapa nyumbani hivyo tunataka furaha,” alitamba kocha huyo.