Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwalwisi aichorea ramani Mbeya Kwanza

MWALWISI Pict

Muktasari:

  • Mbeya Kwanza iliyowahi kucheza Ligi Kuu msimu wa 2021/22 tangu iliposhuka daraja, haijarejea tena licha ya kuonyesha ushindani kwenye Championship ikiwamo kushika nafasi ya 4.

WAKATI Mbeya Kwanza ikiendelea kusota Ligi ya Championship kwa misimu minne sasa, kocha mkuu wa timu hiyo, Makka Mwalwisi amesema iwapo uongozi utazingatia ripoti aliyowasilisha, huenda msimu ujao wakarejea Ligi Kuu.

Mbeya Kwanza iliyowahi kucheza Ligi Kuu msimu wa 2021/22 tangu iliposhuka daraja, haijarejea tena licha ya kuonyesha ushindani kwenye Championship ikiwamo kushika nafasi ya 4.

Katika msimu uliomalizika hivi karibuni, imemaliza nafasi ya saba kwa pointi 50 huku Mtibwa Sugar na Mbeya City zikipanda daraja baada ya kumaliza katika nafasi mbili za juu.

Hata hivyo, katika msimu wa 2023/24, timu hiyo ilimaliza nafasi ya nne ikicheza mchujo ‘Playoffs’ ya kupanda daraja, ambapo ilitolewa na Biashara United kwa jumla ya mabao 4-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mwalwisi alisema kinachoitesa timu hiyo ni kutokuwa na muendelezo wa kutunza wachezaji wenye ubora na ushindani, hali ambayo kwa timu yoyote lazima ipitie magumu.

Malwisi alisema baada ya kumaliza ligi msimu huu, amewasilisha ripoti ikibainisha udhaifu na nini cha kufanya kwa ajili ya msimu ujao, ikiwa ni usajili imara na maandalizi ya mapema.

“Baadhi ya viongozi wa timu zetu hawana kuamini mchakato wa maendeleo, wanapomaliza msimu bila kujali ubora wa mchezaji wanaamua kuacha, maandalizi yanakuwa duni,” alisema Malwisi na kuongeza;

“Niwasilisha ripoti ikibainisha yote na nini kufanyike, ikitekelezwa vyema, Mbeya Kwanza itarudi haraka Ligi Kuu, mpira wa sasa hautaki njia fupi.”

Kocha huyo mwenye rekodi na historia ya kupandisha timu kadhaa ikiwamo Mbeya City, anaongeza kuwa kwa sasa soka la Mbeya limekua.