Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KenGold: Morrison kuvaa uzi wa Simba ni uzalendo

MORRISON Pict

Muktasari:

  • Bosi huyo amesema hata yeye licha ya kuwa shabiki wa Yanga, lakini leo alikuwa upande wa Simba kuwaombea kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo Morrison kuonekana amevaa jezi tofauti na timu yake ni suala la kizalendo.

Uongozi wa KenGold umesema kitendo cha nyota wa timu hiyo, Bernard Morrison kuonekana akiwa na jezi ya Simba ilihali ana mkataba na timu hiyo wanalichukulia kizalendo kwa kuwa Wekundu hao waliwakilisha nchi kimataifa.

Morrison aliyewahi kucheza Yanga na Simba kwa misimu tofauti, alijiunga na KenGold dirisha dogo na hadi sasa bado ana mkataba hadi mwisho wa msimu huu.

Hata hivyo, tayari timu hiyo imeshuka daraja baada ya kudumu msimu mmoja ikivuna pointi 16 ikisaliwa na mechi mbili kufunga msimu wa ligi hiyo.

Katika hali isiyo ya kawaida, Morrison alionekana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar akiwa na jezi ya Simba wakati wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS BerKane ya Morocco, huku akionesha kushangilia akionesha uzi huo jukwaani.

Kama haitoshi katika michezo miwili iliyobaki kwa KenGold kumaliza Ligi, itakutana dhidi ya Simba, Juni 18 mechi ikipigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora kisha kumaliza msimu dhidi ya Namungo.

Mkurugenzi wa timu hiyo, Kenneth Mwakyusa amesema licha ya nyota huyo kuwa ndani ya mkataba, lakini tukio la kuonekana amevaa jezi tofauti na timu yake wanalichukulia kizalendo.

Amesema kwa kuwa winga huyo aliwahi kucheza Simba, huenda bado ana mapenzi na timu hiyo, akibainisha kuwa hata yeye mwenyewe alikuwa anawaombea Wekundu hao kushinda na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo Afrika.

"Mimi mwenyewe ni Yanga, lakini leo nilikuwa upande wa Simba kuwaombea washinde, hivyo tukio hilo japo sijaliona ila naliona kama uzalendo, hapa tunatanguliza utaifa kwanza," amesema Mwakyusa nw kuongeza;

"Halafu isitoshe Morrison kabla ya kuja kwetu alikuwa Simba, kwa hiyo huenda bado ana mapenzi na timu, ndio hali ya wachezaji wetu tulionao."

Katika mchezo huo wa fainali, Simba ikimaliza dakika 90 ikiwa pungufu kufuatia kadi nyekundu ya kiungo Yusuph Kagoma imelazimishwa sare ya bao 1-1 na kufanya wapinzani kutoka Morocco kutwaa taji hilo kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya mchezo wa kwanza kushinda 2-0.