Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuwaombee… Dabi imeshika hatma zao

TUWAOMBEE Pict

JUNI 25 kinapigwa Uwanja wa Mkapa kati ya Yanga dhidi ya Simba mchezo ambao ulipiga kalenda, lakini sasa hakuna kipengele tena ni lazima kiwake.


Mchezo huo weka mbali mambo ya ugumu ulionao, lakini safari hii unakwenda kutoa picha halisi kwamba nani atakuwa bingwa wa msimu huu.


Itakumbukwa awali mechi hiyo ilikuwa ipigwe Machi 8, 2025 lakini ikaahirishwa na kuibua utata juu ya hatma yake, ikapangwa tena ipigwe Juni 15, 2025 nako haikuchezwa na ikaja tarehe mpya ambayo ni Juni 25 saa 11 jioni.

Ndani ya mchezo huo kutakuwa na presha flani hivi kutoka kwa baadhi ya wachezaji ambao hasa ni wale wanaomaliza mikataba ndani ya vikosi hivyo, lolote litakalotokea leo inaweza kuwa ndio tiketi ya kupewa mkono wa kwaheri au kulamba mkataba mpya.


CHE MALONE FONDOH (SIMBA)

Msimu huu ukimalizika beki Che Malone Fondoh atakuwa amemaliza mkataba na tayari ameshakuwa kwenye wasiwasi wa kutoongezwa mkataba mpya kuanzia pale Simba ilipong’olewa na Singida Black Stars kwenye nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).

Che Malone atakuwa sehemu ya mchezo huo na kama ikitokea Simba ikipoteza kisha matokeo hayo yakamhusisha kwamba makosa yalianzia au kupitia kwake, inaweza kuwa hitimisho la raia huyo wa Cameroon kuichezea timu hiyo.


KHALID AUCHO (YANGA)

Kiungo wa shoka wa Yanga pale eneo la ukabaji akicheza kwa ubora mbele ya mabeki wa timu hiyo naye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Ubora alionao na umuhimu wake kikosini ni wa kipekee, lakini kama yakitokea makosa yakapitia kwake hilo linaweza kuwa hitimisho baya kwake licha ya mambo makubwa ambayo ameyafanya kwenye timu hiyo.


MOHAMED HUSSEIN ‘TSHABALALA’ (SIMBA)

Beki na nahodha wa Simba ambaye amekuwa na mwendelezo bora wa kiwango, lakini uhakika ni kwamba anamaliza mkataba mwisho wa msimu huu na hiyo itakuwa mechi ya mwisho kwake.

Tshabalala anayecheza beki wa kushoto anatakiwa kuhakikisha hata kama Simba ikipoteza, basi Yanga isitengeneze ushindi kupitia eneo analocheza kwani hilo litakuwa jambo baya kwake wakati huu inajipanga kumuongezea mkataba.


MUDATHIR YAHYA (YANGA)

Ukiambiwa utaje viungo wawili wakabaji ambao wanaweza kucheza mchezo dhidi ya Simba ndani ya kikosi cha Yanga hutaliacha jina la Mudathir Yahya. Ubora wake unampa nafasi kubwa ya kucheza mechi hiyo.

Mudathir anamaliza mkataba wake ndani ya Yanga msimu huu.  Tayari pande hizo mbili zimepeana makubaliano ya awali kwamba zitaingia mkataba, lakini lolote linaweza kutokea kama timu yake itapoteza na makosa yakianzia eneo analocheza mchezaji huyo.


MOUSA CAMARA (SIMBA)

Kipa namba moja wa Simba ambaye ni uhakika atakuwa golini endapo tu afya yake iko sawa. Unakumbuka mchezo wa kwanza ambao ulimalizika kwa Wekundu wa Msimbazi kulala kwa bao 1-0? Ziliibuka lawama nyingi kufuatia namna alivyookoa shambulizi lililozalisha bao la beki Kelvin Kijili kujifunga.

Camara anamaliza mkataba wake na Simba akiwa amefanya kazi nzuri na kuibuka kuwa kipa bora akiwa na cleen sheet 19 hadi sasa.

Lakini kama itatokea chama lake likipoteza na makosa kuonekana yametokana yeye itatarajiwa kwamba klabu yake kuingia sokoni na kutafuta kipa mpya.


CLATOUS CHAMA (YANGA)

Kuuzwa kwa Stephanie Aziz KI kwenda Wydad Casablanca kabla ya kumalizika kwa msimu na pia hatihati ya mshambuliaji Prince Dube aliyeumia kuwapo mchezoni kunatoa nafasi kwa kiungo Clatous Chama kuwa kwenye uwezekano wa kucheza mchezo wa dabi.

Chama anamaliza mkataba mwisho wa msimu huu akiwa na Yanga na pande hizo mbili zimeshaanza mazungumzo ya kuongeza mwingine, lakini kiwango chake kwenye mechi zilizopita mbili kimekuwa kikubwa akitafuta mkataba mpya na kama ikitokea akacheza kwa kiwango cha kawaida timu yake itapima kama imuongezee au imuache.