Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZILITRENDI: Simba, Yanga zakeshea juju Taifa

TUNAENDELEA kuwakumbushia stori zilizotrendi miaka ya nyuma na leo, Juni 16 tunarudi hadi mwaka 2001 na kukuta habari inayohusu wanachama wa Simba, Yanga kukesha usiku kucha kwenye Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) kuwekeza 'Juju' siku moja kabla ya kukutana.
Mmoja wa wasimamizi wa uwanja huo kwa kipindi hicho, Habir Auckland alisema katika mahojiano maalumu juu ya hali hiyo kwamba wanachama hao hufika uwanjani hapo kwa makundi na kwa nyakati tofauti hadi usiku wa manane.
Auckland alisema wanachama hao wamekuwa wakifanya vitendo mbalimbali vinavyosadikika imani za kishirikina kwenye uwanja huo.
"Sijui ni wapenzi ama wanachama, wamekuwa wakifika hapa kwa makundi na kuvunja nazi na mayai, tena usiku wa manane, sisi tunakuwa sana makini kwani wanaweza kuwa wengine ni vibaka," alisema Auckland.
Aliongeza wakati wingine viongozi wao hufika uwanjani hapo kwa ajili ya kuwakagua 'walinzi wao' kama kazi inaenda barabara.
"Sitaki kuwataja, lakini viongozi tunawaona wanakuja usiku wa manane kukagua kama kazi ya ulinzi inakwenda vizuri pamoja na shughuli za utendaji kama zimefanyika ipasavyo," alisema Auckland.
Imani za ushirikina zimekuwa zikitawala siku zote wakati mahasimu hao wanapokutana ikiwa ni pamoja na kurusha njiwa na kukatiza mara kadhaa katikati ya kiwanja.
Hata hivyo, imekuwa ikidaiwa wakati mwingine kwamba hali hiyo ni 'Tisha Toto' kwa timu nyingine kujua imewekewa juju wakati hakuna lolote.