Watanzania vicheko wakizidi kuneemeka mitandaoni
FURAHA inazidi mioyoni mwa Watanzania ambao wamethubutu na kushiriki katika minada inayoendeshwa mitandaoni kwani wameendelea kujizolea zawadi mbalimbali zenye thamani kubwa.
Katika moja ya minada inaoshika kasi, washindi mbalimbali wametangazwa na kufichua furaha yao akiwamo Joyce Brown (27), mfanyakazi katika kampuni binafsi, amejishindia simu aina ya Samsung Galaxy A06.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Joyce alisema amefahamu kuhusu mnada wa Piku Afrika baada ya kuambiwa na rafiki yake aliyewahi kushinda bidhaa mbalimbali kutokana na jukwaa hilo.
“Nilipoona rafiki yangu ameshinda zawadi, nilihamasika kujaribu bahati yangu. Kwa kweli ni ya ukweli, hakuna ‘janjajanja’.
Nawashauri Watanzania wajitokeze kwa wingi kushiriki, kwani kila mtu ana nafasi ya kushinda,” alisema Joyce kwa furaha.
Witness Saimon (37), mfanyabiashara, amejishindia combo la kike na kiume lenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni.
Amesema rafiki yake ndiye aliyekuwa akimshawishi kushiriki na baada ya kushawishika, hatimaye ameibuka mshindi.
“Ingawa rafiki yangu bado hajashinda, hajakata tamaa.
Anaendelea kushiriki kwa matumaini kuwa siku moja atapata. Napenda kuwapongeza kampuni hii kwa uaminifu wao na namna wanavyowajali washindi wao,” alisema Witness.
Kwa upande wake, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa kampuni hiyo ya mnada mtandaoni, Barnabas Mbunda amesema kampuni hiyo inaendelea kutoa fursa nyingi zaidi kwa washiriki wake katika minada mbalimbali yenye zawadi kubwa.
Mbunda amesema mwisho wa mwaka huu mshindi ataibuka na gari mpya aina ya Toyota Raum, lenye bima ya mwaka mzima na kadi ya mafuta, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh30 milioni.
Pia kutakuwa na mshindi wa mgodi wa Piku na atajinyakulia seti ya dhahabu safi yenye thamani ya Sh6 milioni na atapata nafasi ya kuchagua mwenyewe dukani seti anayoitaka.
Baada ya siku 28, kupitia Zigo la Piku, mshiriki atakayetoa dau dogo na la kipekee atashinda pikipiki mpya aina ya TVS, ikiwa na helmet, reflector, kadi ya mafuta ya miezi sita na bima, vyote vikiwa na thamani ya Sh4 milioni.
Aliongeza kila baada ya siku 14, kwenye Combo zitatolewa saa ya kisasa, manukato ya gharama, pamoja na Televisheni ya LG inchi 55 na Airtel Router iliyolipiwa mwaka mzima, zenye jumla ya thamani ya Sh2.4 milioni.
Mbunda alibainisha hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kupanua wigo wa huduma zake na kuwapa Watanzania nafasi ya kushindania bidhaa kubwa zinazoweza kubadilisha maisha yao.
“Tunawahamasisha vijana na watu wazima kuanzia miaka 18 na kuendelea kushiriki. Unachotakiwa kufanya ni kupakua App katika Play Store kwa watumiaji wa Android au App Store kwa watumiaji wa iPhone,” alisema.
Ameongeza washiriki wanaweza kununua tiketi kwa bei nafuu kuanzia Sh1,000 kwa tiketi 10, Sh5,000 kwa tiketi 50, na Sh10,000 kwa tiketi 100, huku nafasi ya ushindi ikiongezeka kadri tiketi zinavyoongezeka.