Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO - Manara: Manula ameruhusiwa kutoka hospitali, ataanza mazoezi

SIKU moja baada ya kipa wa Simba, Aishi Manula kuumia na kupoteza fahamu alipogongana na mchezaji wa JKT Tanzania kwenye mcho wa Ligi Kuu timu hizo zilipokutana jana katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, uongozi wa klabu hiyo umethibitisha kuwa anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitali.

Msikie 'Haji Manara' kuhusu 'Aishi Manula' | "Atasafiri kuelekea Sudan"

Manula aligongana na mchezaji wa JKT Tanzania, Daniel Lyanga katika dakika ya 67 kisha kuanguka na kufikia kichwa, alipewa huduma ya kwanza kwa dakika kadhaa uwanjani hapo na kuwahishwa Hospitali ya Kairuki kwa matibabu zaidi huku nafasi yake ikichukuliwa na Beno Kakolanya.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari wa Simba, Haji Manara amesema hali ya mchezaji huyo imezidi kuimarika na amezungumza naye akisema maumivu anayasikia kwa mbali.

"Nimezungumza na daktari wa timu pia, Yassin Gembe amethibitisha leo atapata mapumziko na kesho atajiunga na wenzake kwa mazoezi na kuanza safari kwenda Sudan," amesema Manara.

Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kupuuza uzushi kwenye mitandao ya kijamii na kusubiri kumuona kipa huyo namba moja akisafiri na timu kwenda kuwavaa Al Merrikh Jumamosi Machi 6 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika..

Katika mchezo jana Simba ilishinda kwa mabao 3-0 yaliyofungwa na Chris Mugalu, Luis Miquissone na John Bocco aliyeingia kipindi cha pili.