Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida watamba Twende Olimpiki 2024

Nahodha wa timu ya mpira wa wavu ya wasichana ya Mbeya, Alumbeage Ngao. Kulia ni Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau. Mbeya iliifunga Singida katika Tamasha la Michezo la Twende Olimpiki  2024 kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mwenge mkoani Singida jana

MKOA wa Singida umetamba katika Tamasha la Michezo la Twende Olimpiki lililomalizika jana hapa.

Singida walitwaa ubingwa katika soka la wavulana na wasichana baada ya kuwafunga Mbeya kwa mabao 2-1 na 3-0, huku wakizoa medali katika riadha

Mbeya nao hawakutoka mikono mitupu baada ya kushinda michezo ya wavu kwa wavulana na wasichana na hivyo kuondoka na makombe na fedha taslimu.

Mshindi wa kwanza katika michezo ya timu,  kila moja aliondoka na Sh  milioni 1, hivyo Mbeya waliondoka na jumla ya Sh milioni 2.

Katika riadha, Singida walitwaa medali tisa, fedha sita na shaba tano huku Mbeya wakipata dhahabu moja, fedha nne na shaba tano.

Katika mpira wa wavu, Mbeya walitwaa medali za dhahabu mbili, huku Singida nao walitwaa fedha mbili kwa wanawake na wanaume.

Katika soka, Singida walitwaa ubingwa kwa wavulana na wasichana baada ya timu zao kushinda katika fainali.

Katika riadha mshindi wa kila michezo kwa wavulana na wasichana,  kila mmoja alipata Sh 300,000, wa pili Sh 200,000 na watatu Sh 100,000.

Tamasha hilo lilifanyika katika Shule ya Sekondari Mwenge lilifunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego na kuhungwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe.

Tamasha hilo liliandaliwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na kudhamiliwa na Ubalozi wa Ufaransa Tanzania.