Mtoano Uefa...waache wauane
NYON USWISI: MWISHO wa maneno maneno umefika. Ndicho unachoweza kusema baada ya droo ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ya 16 bora kupangwa, huku Arsenal ikipewa bingwa wa zamani wa michuano hiyo.
Manchester City yenyewe wamepewa timu iliyoku-wa kundi moja na mahasimu wao, Manchester United, FC Copenhagen, hivyo itakuwa ni mwendo wa kuwaonyesha wapinzani wao wameshindwaje kushinda mechi zao.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta mwenye ndoto ya timu yake kufanya kweli kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, amepanga kumenyana na mabingwa mara mbili wa Ulaya, FC Porto.
Kikosi cha sasa cha Arsenal hakina uzoefu wa hatua hiyo ya mtoano, ambapo mara ya mwisho The Gun-ners kuwamo kwenye 16 bora ilikuwa mwaka 2017, chini ya kocha Arsene Wenger. Safari hii, Arsenal il-iongoza kundi lake, lililokuwa na timu za PSV, Lens na Sevilla.
Wakati huo, Man City yenyewe imepata ukomavu wa michuano hiyo, ikicheza mechi za fainali kwa misimu miwili mfululizo, ikiingia kwenye timu chache za England zilizowahi kufanya hivyo sam-bamba na Nottingham Forest mwaka 1979 na 1980, ambapo ilishinda ubingwa kwa misimu miwili mfululizo.
Mara ya mwisho, Man City kushindwa kufuzu hatua ya 16 ilikuwa msimu wa 2016/17, msimu wake wa kwanza kocha Pep Guardiola baada ya kutua kwenye kikosi hicho cha Etihad. Man City iliongoza kundi lake lililokuwa na timu za RB Leipzig, Young Boys na Red Star.
Utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya haijaishia hapo, Real Madrid yenye huduma ya staa matata kabisa, Jude Bellingham yenyewe itakipiga na RB Leipzig ya Ujerumani kwenye hatua hiyo ya mtoano, huku Bayern Munich chama la straika Harry Kane itaku-wa na kasheshe la kuwakabili Lazio. Mambo ni mo-to.
Kwenye hatua hiyo ya mtoano kutakuwa na kipute kingine cha kibabe kabisa kitakachohusisha ma-bingwa wa msimu uliopita kwenye Serie A na La Liga, ambapo Napoli watamaliza ubishi na Barcelo-na. Paris Saint-Germain ya Kylian Mbappe yenyewe itakipiga na Real Sociedad, huku Borussia Dort-mund itaanzia ugenini kukipiga na PSV ya Uholan-zi, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu, kipute cha Inter Milan na Atletico Madrid ya kocha Diego Sim-eone na supastaa, Antoine Griezmann.
Mechi za kwanza za hatua hiyo ya mtoano, zitapig-wa Febrauri 13, 14, 20 na 21, wakati zile za marudi-ano zitapigwa Machi 5, 6, 12 na 13 mwakani. Waache wauane.