Mastaa Yanga nje wakiisikilizia Belouizdad

Yanga imewakwepa kiaina wapinzani wake, CR Belouzidad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuanzisha kikosi ambacho hakina mastaa wakubwa kwenye mchezo wa Kombe la Shrikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Polisi Tanzania.
Yanga inacheza na Polisi kwenye mchezo wa raundi ya 32 bora unaoanza saa 1:00 huku kikosi kilichotajwa kikiwa bila nyota wake wakubwa.
Kikosi cha Yanga kinaanza bila kipa namba moja, Djigui Diarra mabeki, Dickson Job na Ibrahim Bacca viungo Pacome Zouazou, Maxi Nzegeli pamoja na beki Yao Kouassi wakiwa wamewekwa jukwaani ili kujiandaa kwa mchezo dhidi ya Belouzidad, Jumamosi ijayo.
Hii ina maana kwamba kama wapinzani hao wa Yanga wametuma mashushushu kwenye mchezo huo ili kuitazama timu hiyo inavyocheza, watakuwa wamepotea vibaya kwa kuwa Jumamosi watakutana na watu wengine tofauti.
Kikosi cha Yanga kilichoanza kina mastaa watatu tu ambao wamecheza mechi nyingi msimu huu, Aziz Ki, Joyce Lomarisa na Bakari Mwamnyeto.

Hata hivyo, hii itakuwa mechi ya mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joseph Guede kuonyesha uwezo wake akiwa ameanza kwenye nafasi ya ushambuliaji.
Staa huyo tangu ametua nchini bado hajawaridhisha mashabiki baada ya kucheza michezo mitano bila kufunga bao.

Kikosi kilichoanza cha Yanga kinaongozwa na Abutwalib Mshery,
Kibwana Shomary, Joyce Lomalisa, Gift Fred, Bakari Mwamnyeto, Gift Mauya, Agustine Okrah, Jonas Mkude, Aziz Ki na Farid Mussa.