Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabao anayofungwa Shikhalo daaah!

Muktasari:

KWANI Shikhalo mwenyewe anasemaje! Pengine atatoa majibu ya shida inayoonekana kumwandama kipa huyo wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufungwa mabao ya umbali mrefu.

KWANI Shikhalo mwenyewe anasemaje! Pengine atatoa majibu ya shida inayoonekana kumwandama kipa huyo wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufungwa mabao ya umbali mrefu.

Juzi Jumapili kwenye mchezo wa ligi hiyo, Yanga ilipokubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC, kipa Faruk Shikhalo alijikuta akifungwa na Prince Dube kwa bao la staili hiyo hiyo ya kutoka umbali mrefu.

Kuna nini? Kwa Shikhalo tatizo hilo la kufungwa mabao ya mbali linaonekana linaanza kuota mizizi kutokana na kuruhusu nyavu zake kuguswa kwa staili hiyo ya mabao zaidi ya mara moja katika mechi za hivi karibuni.

Mchambuzi maarufu wa mchezo wa soka, Mwalimu Alex Kashasha aliliambia Mwanaspoti kuwa Shikhalo anatakiwa afanye mazoezi ya spidi, unyumbufu, hesabu na uokoaji wa mipira ili aepukane na adha ya kufungwa mabao ya aina moja mara kwa mara.

Ushauri huo kwa Shikhalo umetolewa siku moja baada ya kipa huyo kufungwa bao la mbali na straika wa Azam, Dube ambapo shuti lake halikuonekana kuwa tishio sana, lakini haikuwa hivyo kwa kipa huyo raia wa Kenya na kujikuta akiokota mpira nyavuni.

“Nilichokiona kwa lile bao ni kwamba Shikhalo hana spidi na ni mzito kufanya hesabu na makadirio hayaendi sawa. Anakosa pia unyumbufu hali inayosababisha ‘timing’ isiwe nzuri,” alisema Kashasha na kuongeza:

“Dube alipiga ule mpira akiwa nje ya eneo la hatari na ukampita Shikhalo karibu na alipokuwepo. Kama angekuwa na hesabu nzuri angeweza kuuokoa. Mipira kama ile ndio huwa inawafanya makipa wajizolee sifa kwa sababu pale ama alitakiwa kuukamata au kuuondosha kwa kuangalia mpira unatokea upande gani.”

Bao hilo la Dube ni la tano kwa Shikhalo ndani ya msimu huu kufungwa kwa mashuti ya mbali, kuna mechi kadhaa huko nyuma amekuwa akiruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mtindo wa mabao hayo.

Mechi ambazo kipa huyo ameruhusu mabao ya mbali tofauti na ya juzi dhidi ya Azam FC ni dhidi ya timu za Gwambina, Prisons, KMC na Coastal Union.

Hata hivyo, kocha wa makipa wa Yanga, Razack Ssiwa amemtetea Shikhalo na kusema mfungaji ndiye anatakiwa kusifiwa badala ya watu kumlaumu kipa huyo.