Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam: Huyu Carlinhos balaa

Muktasari:

KAMA Yanga wanamtafuta mchawi nani baada ya kupoteza dhidi ya Azam FC, basi kocha msaidizi wa Azam, Bahati Vivier amefichua kwamba mabadiliko ya kumtoa Carlos Carlinhos yaliwapa nafasi wao kucheza mpira.

KAMA Yanga wanamtafuta mchawi nani baada ya kupoteza dhidi ya Azam FC, basi kocha msaidizi wa Azam, Bahati Vivier amefichua kwamba mabadiliko ya kumtoa Carlos Carlinhos yaliwapa nafasi wao kucheza mpira.

Carlinhos alitoka dakika 78 na kuingia Haruna Niyonzima katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa juzi Jumapili ambapo Azam walishinda bao 1-0 huku mabadiliko hayo yakichangia kuizamisha Yanga baada ya Niyonzima kuupoteza mpira miguuni kwa Aggrey Morris, ambaye alipiga pasi ndefu iliyotua kwa muuaji Prince Dube, ambaye alipiga shuti la mbali na kufunga bao la kideoni.

Vivier alisema Carlinhos aliwanyima kucheza mpira lakini alipotolewa iliwafanya wawe huru kucheza mpira kama walivyotaka. “Alipokuwepo yeye uwanjani tulikuwa tunapata kazi kumkaba, lakini alipotoka tulimuweza Mukoko na kumfanya asicheze na tulifanikiwa,” alisema.