General Sport’s yang'ara Chipkizi 2023
TIMU ya General Sports kutoka jijini Dar es Salaam imeng'ara katika michuano ya Kombe la Chipkizi 2023 kwa vijana yaliyofanyika Arusha.
Katika michuano hiyo General Sports iliibuka mabingwa kwa mikwaju ya penalti 9-8, dhidi ya Bulls Girls huku kwa upande wa Wanaume ikimaliza mshindi wa pili baada ya kupoteza kwa penalti 6-5 mbele ya Suluhu Academy kutoka visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Mwanaspoti Online muasisi wa timu hiyo, Amocha amesema licha ya kutochukua ubingwa kwa Wanaume ila kwao ni mafanikio makubwa huku akiwapongeza wadhamini wao, Duka Direct na Selcom waliochangia mafanikio yao hadi walipofikia.
"Sio kwa kiwango kikubwa lakini tunashukuru kwa hapa tulipofikia kwani tumeona vipaji vingi ambavyo kama vitaendelezwa basi tutakuwa na kizazi bora cha baadae, kikubwa ni kuendelea kuwapa hamasa vijana tukitambua mpira ni ajira," amesema.
Michuano hiyo iliyomalizika ilikuwa ikishirikisha timu nyingi kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda na Congo ambapo imehusisha watoto wa kiume na wa kike kutoka ndani na nje ya nchi wenye umri kuanzia miaka saba na 20.
Hiyo ni ishara nzuri kwa kikosi hicho kwani mara ya mwisho kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano hayo ilikuwa ni 2021 kwa wanawake chini ya miaka 15 huku mwaka jana ikishindwa kufurukuta na kuishia ikitupwa nje kwenye hatua ya nusu fainali.