Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi amkomalia Guede

Muktasari:

  • Hivi unavyosoma Mwanaspoti tambua kwamba straika huyo mpya yupo katika hatua za mwisho kutua nchini wakati wowote kuanzia leo ili aungane na wenzake kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi hizo muhimu.

Yanga inaendelea kujifua kwa ajili ya kumalizia viporo vya mechi za Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na michezo ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ameamua kumkomalia straika mpya Joseph Guede kutoka Ivory Coast.

Hivi unavyosoma Mwanaspoti tambua kwamba straika huyo mpya yupo katika hatua za mwisho kutua nchini wakati wowote kuanzia leo ili aungane na wenzake kambini kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mechi hizo muhimu.

Hatua ya kuwahi kwa Guede imetokana na uamuzi wa Gamondi kuamua kumuita haraka kikosini mshambuliaji huyo raia wa  Ivory Coast ili aje aanze kuzoeana na wenzake.

Gamondi alisema kila mchezaji ambaye hayupo katika vikosi vya timu za taifa kwenye michuano ya Afcon  anapaswa kuwa katika kikosi hicho kilichopo kwenye mazoezi ambapo pia Gueye amemuita haraka.

Kocha huyo alisema Guede anatakiwa kuja kufanya maandalizi haraka na wenzake ambayo yatamrahisishia kuwa na mwanzo mzuri ndani ya timu hiyo wakati wa mashindano utakaporejea.

“Tunaendelea na mazoezi yetu hii wikiendi tulipumzika kidogo kazi zaidi itaendelea Jumatatu (kesho) ni muhimu kuwa tayari mapema nafurahia jinsi wachezaji wanavyojituma licha ya ugumu wa ratiba ya mazoezi,” alisema Gamondi na kuongeza:

“Kwa sasa kila mchezaji ambaye hayupo na timu ya taifa tupo naye kasoro kijana wetu Guede. Nimeongea naye nimemwambia umuhimu wa kuwahi haraka kuja kuanza kazi. Anahitaji kuanzia hapa ambako tunafanya Sasa ili imsaidie kuwa sawa na wenzake, naamini atafika kama ambavyo tumezungumza, hatuna shida sana na Hawa ambao wako timu za taifa kwa kuwa wao wanapata mazoezi ya kutosha.”

Yanga ina mechi mbili za viporo vya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mashujaa na Tanzania Prisons, pia akiwa na kiporo cha michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Hausing ya Njombe, huku kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika itacheza na CR Belouzdad ya Algeria Februari 23 jijini Dar es Salaam kisha kuifuata Al Ahly ya Misri katika mchezo utakaopigwa Machi Mosi.

Hadi sasa timu hiyo inashika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu nyuma ya Azam na ipo ya pili katika Kundi D nyuma ya Ahly zikiwa zimelingana pointi tano kila moja, licha ya Wamisri kuwa na mchezo mmoja mkononi.