Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dogo Mtanzania awasapraizi Warussia

Muktasari:

Misonge anashiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya Games of the Future ambayo yalianza Jumatatu wiki hii jijini Kazan, Russia.

KINDA wa Kitanzania, Harrith Chunga ametajwa kuwa kivutio katika mashindano ya Games of the Future yanayoendelea Russia.

Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka yakishirikisha watoto kutoka zaidi ya nchi 120, yanalenga kuibua vipaji na kuviendeleza katika michezo tofauti na stadi za maisha.

Kiongozi wa timu ambayo kinda huyo wa Kitanzania amepangwa katika mashindano hayo, Anzhelika Markovich amesema Chunga ameonyesha tabia za kipekee hivyo wanaamini atakuja kuwa mwanamichezo mwenye jina kubwa duniani.

"Ni kijana mzuri sana na napenda sana kumtazama na anafurahia maisha yake. Anatupa hisia nzuri sana pindi anapocheza au kufanya majukumu aliyopewa na kiukweli ni wa kipekee.

"Anajitahidi kumudu mazingira na anacheza vizuri na anaonekana ni mweledi, naamini anaweza kufika mbali," alisema Markovich.

Katika mashindano hayo, watoto wanapata fursa ya kushiriki katika michezo 16 tofauti na wanagawanywa katika makundi ya watoto watano kila moja ili kupata washindi.

Hiyo ni mara ya pili kwa Harrith Chunga kushiriki mashindano makubwa ya michezo duniani na mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana aliposhiriki mashindano ya soka ya Gothia yaliyofanyika Sweden.

Mashindano ya Games of the Future hufanyika kila mwaka Russia yakishirikisha watoto kutokea maeneo tofauti duniani na yalianzishwa rasmi mwaka 2009.

Vipengele vitano tofauti hutazamwa katika kupata washindi wa mashindano hayo ambavyo ni michezo, mbinu, ufundi, mapambano ya mwili na kukimbia kwa kasi.