Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba ampa Saido mbinu mpya

BABA mzazi wa staa wa Yanga, Saido Ntibazonkiza amepagawa na kiwango cha mwanaye anachokionyesha ndani ya klabu hiyo na akamuongezea mbinu.

Mzazi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Burundi pia ana mtoto mwingine anayecheza Namungo, Stive Nzigamasabo anayevaa jezi namba 10.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kituo kimoja cha Burundi, mzazi huyo ameweka wazi kwamba huwa anamfuatilia mchezaji huyo kila anapocheza na tayari ana uzi wa Yanga.

Ili azidi kufanya vizuri zaidi amempa mbinu mpya ikiwemo kuzidisha zaidi mazoezi binafsi, kujituma kwa kiwango cha juu zaidi pamoja na kumheshimu kocha na viongozi. “Akiingia uwanjani ajitume zaidi kupata mafanikio makubwa kwa vile ile ni kazi anafanya, nawaombea vijana wangu wafanye vizuri zaidi,” alisema.

Mzee huyo amesisitiza kuwa kwa sasa yeye ni shabiki wa Yanga na anavaa jezi ya klabu hiyo kila mahali.

“Kila Saidi alikocheza mimi jezi ninayo, mimi sasa na Yanga siwezi kushangilia timu nyingine. Mimi ni Yanga, Saidi alipoingia Yanga nimekuwa Yanga damu, niko Yanga damu,” alisema huku akisisitiza kuwa anafuatilia kila mechi ya Yanga kwenye televisheni na mitandao ya kijamii. Saidi ametokea kung’ara ndani ya kikosi cha Yanga tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo kama mchezaji huru. Saido amefunga mabao mawili na kuasisti matatu ndani ya Ligi Kuu Bara.