Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanufaika minada mtandaoni wazidi kumiminika

ISHU Pict

Muktasari:

  • Baadhi ya Watanzania wamejishindia fedha na bidhaa kutokana na promosheni ya kidijitali na kuonyesha kufurahia matumizi ya mitandao kwa kuwapa faida huku wakihimiza na wengine wajiunge na minada hiyo.

WAKATI ndiyo huu kwa Watanzania kuendelea kunufaika na mitandao ya kijamii kama wanavyofaidika baadhi kutokana na majukwaa mbalimbali yanayotoa zawadi za fedha na bidhaa mbalimbali ya minada ya kidijitali.

Baadhi ya Watanzania wamejishindia fedha na bidhaa kutokana na promosheni ya kidijitali na kuonyesha kufurahia matumizi ya mitandao kwa kuwapa faida huku wakihimiza na wengine wajiunge na minada hiyo.

Walioshinda zawadi hizo kutoka kampuni ya minada kidijitali ya Piku Afrika iliyoendesha promosheni ya awamu ya nne ni Hamimu Madenge aliyejishindia bidhaa zenye thamani ya Sh2 milioni, mshindi wa pili, Adam Ahmad, mkazi wa Goba na muuzaji wa vifaa vya ujenzi, amejishindia simu janja aina ya Samsung, laini ya Airtel yenye kifurushi cha mwaka mzima pamoja na spika.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi zake, Madenge amesema alilifahamu jukwaa hilo kupitia mteja wake mmoja wa dukani na alipomwelekeza jinsi ya kucheza alivutiwa na mnada huo Kisha kuamua kushiriki kwa dhati akiamini lazima ashinde.

"Nilipoanza kucheza nilijiambia moyoni hapa si jaribio, bali lazima nishinde. Niliweka fedha, nikapata tiketi za kutosha na kushinda baadhi ya bidhaa zilizokuwepo katika mnada. Nimepokea zawadi zangu, hakika ni nzuri na zina ubora wa hali ya juu," amesema Madenge.

Ahmad amesema alilifahamu jukwaa hilo la mnada kupitia rafiki yake ambaye alijiunga nalo na kushinda hivyo aliamua na yeye kucheza ili ajipatie zawadi. 

“Nilipojaribu nami nikabahatika kushinda simu ambayo nilikuwa nahitaji. Hili jukwaa si wadanganyifu, ni wa kweli kabisa, ukishinda unapewa bidhaa zako. Nawashauri watu washiriki na wao watajishindia," amesema.

Kwa upande wa tiketi za kushiriki, jukwaa hilo limeweka viwango rahisi kama ifuatavyo, tiketi 10 kwa Sh1,000, tiketi 50 Sh5,000, tiketi 100 kwa Sh10,000 na tiketi 1,000 kwa Sh100,000.

Akizungumzia promosheni hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa jukwaa hilo, Barnabas Mbunda amesisitiza kadri idadi ya tiketi inavyoongezeka, ndivyo nafasi ya kushinda inavyokuwa kubwa zaidi.

“Ili kuweza kuingia katika mnada huu unatakiwa kupakua App ya Piku katika play store au Apple Store, Kisha kufuata maelekezo, niwashauri watu waendelee kujiunga na kucheza kwani bidhaa za kushindaniwa bado zipo nyingi,” amesema.

Mbunda ameongeza minada mikubwa inaendelea kushindaniwa ikiwemo gari aina ya Toyota Raum, Pikipiki mpya aina ya TVS pamoja na dhahabu.

Kwa mara nyingine, jukwaa hili limeonesha kuwa kinara katika mapinduzi ya minada ya mtandaoni nchini, ikiwapa Watanzania fursa ya kupata bidhaa bora kwa bei nafuu kutokana na mfumo wa kidijitali, wa uwazi na wa kipekee.
@@@