Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ebwanaeee... Ngoma za hawa zilivuma sana Bongo

JAMAA Pict

Muktasari:

  • MIAKA ya 2000 ilikuwa kipindi ambacho muziki wa Tanzania Bongo Fleva ulishika kasi sio ndani pekee bali hadi Afrika Mashariki na Kati. Hata hivyo, mbali na wasanii wa ndani, kulikuwa pia na wasanii wa nje waliovuma kwa kiwango kikubwa nchini na kuonekana kama sehemu ya mapinduzi makubwa katika muziki huo.

MIAKA ya 2000 ilikuwa kipindi ambacho muziki wa Tanzania Bongo Fleva ulishika kasi sio ndani pekee bali hadi Afrika Mashariki na Kati. Hata hivyo, mbali na wasanii wa ndani, kulikuwa pia na wasanii wa nje waliovuma kwa kiwango kikubwa nchini na kuonekana kama sehemu ya mapinduzi makubwa katika muziki huo.

Wimbo ukipendwa Tanzania, ulikuwa unatawala mitaa, redio na klabu mbalimbali na wasanii wengine hadi leo ngoma zao zinafanya vizuri.

Hivyo basi, majina makubwa kama Koffi Olomide, Fally Ipupa, Awilo Longomba, Chameleone na wengineo yalitikisa anga za Bongo kwa ngoma zao zilizochanganya mitindo ya Kikongo, Naija Pop, na R&B.

Nyimbo zao ziliunganishwa haraka na ladha ya Watanzania, wengine wakitumia Kiswahili na ngoma zao zilikuwa na ujumbe ambao ilikuwa rahisi kuwafikia Watanzania.

Mwanaspoti linakuletea baadhi ya wasanii wa nje ambao walikubalika na ngoma zao zilifanya vizuri na nyingine hadi leo zinaendelea.

JAMA 01

1. Jose Chameleone (Uganda)

Ni mmoja wa wasanii kutoka Uganda ambao walibahatika kupendwa Bongo kutokana na utunzi wake wenye mchanganyiko wa utamaduni wa Kiganda, Ragga, Zouk akitumia lugha ya Kiswahili.

Joseph Mayanja maarufu Chameleone alianza muziki kama DJ katika klabu ya Missouri mwaka 1990. Moja kati ya nyimbo za kwanza ulikuwa wa Bageya aliomshirikisha msanii kutoka Kenya, Redsun.

Albamu yake ya kwanza ilitolewa nchini Kenya mwaka 1999. Tangu wakati huo aliachia albamu kadhaa zikiwa pamoja na Bageya ya 2000, Mama Mia ya 2001, Njoo Karibu wa 2002, The Golden Voice ya 2003, Mambo Bado ya 2004 na Kipepeo ya 2005.

Ngoma zake zilizojaa ujumbe kwa jamii zilimfanya Chameleone kupendwa zaidi Afrika Mashariki na Kati na kuwa mmoja wa wasanii maarufu waliopiga pesa wakati huo.

Nyimbo kama Jamila, Shida za Dunia kutoka kwenye albamu ya Kipepeo iliyotoka mwaka 2005, Badilisha, Tubonge na nyinginezo zilimuweka kwenye ramani na kuwa nyota mkubwa Afrika.

Kila ngoma aliyotoa iliwalenga kundi fulani. Mfano Kipepeo ilikubaliwa zaidi na watoto kutokana na aina ya utunzi aliyoiweka ndani yake.

Ingawa kwa sasa hafanyi muziki kwa asilimia kubwa kutokana na ugonjwa uliomkumba miezi michache iliyopita, bado muziki wake unaendelea kuishi Bongo.

Baadhi ya kolabo alizowahi kufanya na wasanii wa Tanzania ni Mama Rhoda aliyomshirikisha Bushoke na Ndivyo Sivyo aliyofanya na Professor Jay.

JAMA 03

2. Juliana Kanyomozi (Uganda)

Mwanadada huyo kwa sasa anatamba na wimbo wa Yongeza ambao unafanya vizuri na kushika chati mbalimbali za muziki nchini Uganda.

Wimbo uliomtambulisha Bongo ni ule wa mapenzi Usiende Mbali aliomshirikisha Bushoke, kolabo iliyotoka mwaka 2007.

Mtaalamu wa kuandika mashairi ya mapenzi, Bushoke ndiye aliyeuchora wimbo huo mwanzo mwisho na ukafanya vizuri Afrika Mashariki na Kati na kumuongezea jina Kanyomozi ambaye awali hakuwa anajulikana Bongo.

Wimbo huo ukaendelea kufanya vizuri na mwaka uliofuata ukashinda tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kama wimbo bora wa Zouk na hadi sasa ndio ngoma ya Juliana iliyofanya vizuri zaidi YouTube ikiwa na watazamaji milioni 14.

Kolabo na Bushoke ikamfanya msanii kutoka Kenya Kidum kushirikiana na Kanyomozi kwenye ngoma ya Haturudi Nyuma ambayo nayo ilifanya vizuri.

Bado hadi sasa wimbo huo unafanya vizuri Tanzania hasa kwenye vipindi vya redioni na sehemu zingine.

JAMA 04

3. Nyota Ndogo (Kenya)

Jina lake halisi ni Mwanaisha Abdalla maarufu kama Nyota Ndogo, ni mwanamuziki kutoka Kenya ambaye huimba nyimbo za pop ambazo zimechanganywa na taarab.

Anatokea Mombasa ambako ndio muziki wa taarab unafanywa kwa asili kubwa na haikuchukua muda muziki wake ukapendwa Tanzania.

Alianza kuimba miaka ya 2000 lakini wimbo wake wa Watu na Viatu ulimtambulisha kwenye soko la Afrika Mashariki na Kati kutokana na wimbo huo kubeba ujumbe mzito wa marafiki.

Hadi sasa bado unaendelea kufanya vizuri licha ya mwenye wimbo kusahaulika, lakini ujumbe uliokuwa kwenye wimbo huo uligusa hasa marafiki ukisisitiza kuwa mtu wako wa karibu anafurahia ukiwa hauna maendeleo.

Wimbo wake wa Watu na Viatu uliteuliwa kama wimbo bora wa Afrika Mashariki mwaka 2007 katika tuzo za muziki za Tanzania, wimbo huo ukamfanya kuteuliwa na kunyakua tuzo ya msanii bora wa kike Kenya katika tuzo za PAM.

Kwenye moja ya mahojiano ambayo aliwahi kufanya, msanii huyo anayejishughulisha na biashara ya chakula alisema muziki kwa sasa umekuwa mgumu kutokana na mabadiliko ya miziki tofauti.

“Muziki umebadilika, sisi naweza kusema tulikuwa wanamuziki wa zilipendwa kwa sababu sasa hivi nikiimba muziki watoto wadogo hawatujui. Naweza kuimba mwezi mzima na nyimbo haisikiki. Sisi tulipata umaarufu kwa wakati wetu na Tanzania yote niliimaliza.”

JAMA 02

4. Koffi Olomide (DRC Congo)

Antoine Christophe Agbepa Mumba maarufu Koffi Olomide amekuwa muda mrefu kwenye muziki wa Afrika akitajwa kama mmoja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa.

Alianza kupata umaarufu miaka ya 90 na aliendelea kupata mashabiki baada ya kufanya tamasha la kwanza Tanzania mwaka 1999 na baadaye akaenda Kenya ambako nako alijizolea watu.

Tangu aanze kuimba mwaka 1977 bado mkali huyo wa Rhumba ameendelea kuvuma hadi sasa ngoma zake zikichezwa sehemu mbalimbali za starehe.

Licha ya kuimba lugha ya Kilingala na kuchanganya Kifaransa ameendelea kueleweka Tanzania kutokana na aina yake ya uandishi na haikuwa ngumu kufahamika.

Muziki wa rhumba na soukous ulikuwa na mashiko makubwa Afrika Mashariki tangu enzi za Tabu Ley, Franco na baadaye Koffi. Midundo yake ilieleweka kirahisi, haikuhitaji watu kufahamu lugha ili kufurahia.

Koffi na bendi yake Quartier Latin wana miondoko na densi zinazowavutia. Baadhi ya ngoma zake nyingi zimekuwa zikichezwa kwenye klabu mbalimbali na kuwavutia wasikilizaji wasioelewa maneno.

Watoto wa buku mbili wanaweza wasielewe lakini katika miaka ya 1990 redio na baa nchini Tanzania zilipiga sana nyimbo zake kama Loi, Papa Ngwasuma na Effrakata na huu ulimpa jina kubwa nchini.

Tanzania Koffi amefanya kolabo na wasanii kama Diamond Platnumz akimshirikisha mara mbili kwenye wimbo wa Achii na Waah, na Leo Leo akiimba na Nandy.

JAMA 05

5. Sanaipei Tande (Kenya)

Jina lake alilozaliwa ni Natasha Sanaipei Tande maarufu Sanaipei Tande. Mbali na kuimba ni mwandishi na muigizaji.

Mkenya huyo mwenye sauti ya kipekee alianza uimbaji mwaka 2004 na bado anaendelea kufanya muziki wake, ambapo umaarufu mkubwa aliupata Tanzania.

Wimbo kama Kwaheri, Amina, Najuta na Geti Kali ni miongoni mwa ngoma zilizompa umaarufu mkubwa Bongo. Nyimbo zake nyingi ziligusa hisia za watu kwa mashairi ya mapenzi jambo ambalo ndio kiini cha muziki wa Bongo Fleva.

JAMA 06

6. Fally Ipupa (DRC Congo)

Ni miongoni mwa wasanii kutoka DRC Congo ambao waliwahi kutikisa Tanzania na kupata mashabiki wengi kuanzia miaka ya 2006 alipoanza solo career yake baada ya kutoka kwenye bendi ya Koffi Olomide (Quartier Latin).

Ngoma zenye midundo ya Rhumba, Soukous na R&B, mkali huyo wa kibao cha Mayday aliweka ladha ya kisasa kwenye rhumba ya Kikongo, jambo lililowavuta vijana wa Tanzania.

Nyimbo zake za mapenzi zilipendwa Bongo. Alikuwa na hits nyingi kama Orgasy, Kidiambo na baadaye Sweet Life (La vie est belle) na hadi sasa ngoma hizo zinaendelea kufanya vizuri redioni.

Vijana wa Gen Z wanaweza wasielewe lakini mkali huyo anafanya balaa anapokuwa jukwaani kwani hatumii nguvu kucheza, lakini anachokifanya mashabiki wamekuwa wakiinjoi.

Wasanii wengine ni Jean Pierre Nimbona maarufu Kidum, raia wa Burundi, ambaye alijipatia umaarufu baada ya kufanya kolabo na Komando Lady Jaydee Nitafanya.