Alliance v Ceasiaa vita ya 'Top 5' WPL ACHANA na vita ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake kati ya JKT Queens na Simba Queens, kuna mchuano mwingine mkali wa kuwania nafasi ya tano kati ya Alliance Girls na Ceasiaa Queens.
Winga Mbongo atambulishwa Ujerumani WINGA wa Kitanzania, Emma Lattus ametambulishwa kwenye kikosi cha timu ya Borussia Monchengladbach inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Ujerumani akitokea FC Koln 2.
Kocha KMC, Mubesh aona mwanga Ligi Kuu KOCHA wa KMC, Adam Mbwana Mubesh, amesema ameona mwanga tangu aanze kukinoa kikosi hicho, huku akisema kilichobadilika kwa sasa ni mipango tu na anafurahia ushindi alioupata dhidi ya Tabora United.
Gets Program yaungana na Mlandizi HATIMAYE Gets Program imeungana na Mlandizi Queens kushuka daraja Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kukusanya pointi 10 kwenye mechi 17.
Kisa kuikimbia JKT, Fountain kukutana na rungu BAADA ya Fountain Gate Princess kugomea kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake juzi dhidi ya JKT Queens, itakumbana na adhabu ya kutozwa faini ya Sh 2 Milioni na kupokonywa ushindi.
Mynaco ataja ugumu Ligi ya Wanawake nchini Misri KIUNGO wa Zed FC inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Misri, Maimuna Hamis 'Mynaco' amesema msimu huu umekuwa bora kwake kutokana na ushindani ulioongezeka kwenye ligi hiyo.
Chama la Kelvin John hatihati kushuka daraja IMESALIA mechi moja kujua hatma ya chama la mshambuliaji wa Kitanzania, Kelvin John kushuka daraja rasmi.
Novatus asaka rekodi ya Samatta Ulaya MBWANA Samatta anajiandaa kuandikia historia binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushiriki michuano ya Ulaya zaidi ya mara moja baada ya timu yake ya PAOK FC ya Ugiriki kushindwa kufuzu Ligi ya...
Haji Mnoga asaini mwaka mmoja England BEKI wa Salford City na timu ya Taifa, Taifa Stars, Haji Mnoga ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kusalia katika kikosi hicho kinachoshiriki League Two (daraja la nne) nchini England.
Ubingwa WPL... Yanga yatibua hesabu za Simba KIPIGO cha mabao 2-0 ilichopata jioni hii Yanga Princess mbele ya JKT Queens kimetibua hesabu za watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Simba Queens katika mbio za ubingwa kwa msimu huu.