Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Kelvin John hatihati kushuka daraja

KELVIN Pict

Muktasari:

  • John anayekipiga Aalborg Ligi Daraja la Kwanza nchini Denmark timu yake iko mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi 24, sawa na Lyngby ikiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

IMESALIA mechi moja kujua hatma ya chama la mshambuliaji wa Kitanzania, Kelvin John kushuka daraja rasmi.

John anayekipiga Aalborg Ligi Daraja la Kwanza nchini Denmark timu yake iko mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi 24, sawa na Lyngby ikiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mechi ya mwisho dhidi ya Lyngby itakayopigwa Mei 24 itaamua chama la Mtanzania huyo kubaki Ligi Daraja la Kwanza ama kushuka.

Kiujumla kila timu kwenye ligi hiyo inacheza mechi 22 kumaliza msimu na timu mbili zitakazomaliza mkiani zinacheza mechi 10 za mtoano (Play-off) ili kubaki katika ligi hiyo.

Mshambuliaji huyo kabla ya kujiunga na Aalborg aliichezea Genk ya Ubelgiji alikoitumikia pia nahodha wa Stars, Mbwana Samatta.

Msimu huu mshambuliaji huyo amecheza mechi 22 za mashindano yote akiwa na asisti moja na hana bao akicheza dakika 702.