Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mynaco ataja ugumu Ligi ya Wanawake nchini Misri

MYNACO Pict

Muktasari:

  • Mynaco alijiunga na timu hiyo msimu wa 2023 akitokea Yanga Princess ambayo ilimuuza kwenda nchini Misri.

KIUNGO wa Zed FC inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Misri, Maimuna Hamis 'Mynaco' amesema msimu huu umekuwa bora kwake kutokana na ushindani ulioongezeka kwenye ligi hiyo.

Mynaco alijiunga na timu hiyo msimu wa 2023 akitokea Yanga Princess ambayo ilimuuza kwenda nchini Misri.

Kiungo huyo wa zamani wa Simba Queens, Yanga Princess na JKT Queens huu ni msimu wake wa pili kuitumikia timu hiyo na amekuwa muhimu kwenye kikosi hicho ambacho kimekuwa kikimtumia kwenye nafasi mbalimbali za kiungo.

Akizungumza na safu ya Nje ya Bongo, Mynaco alisema ongezeko la timu mbili za Al Ahly na Pyramids limeleta ushindani mkubwa kwenye ligi hiyo.

"Msimu ulikuwa mgumu na wa upinzani mkubwa sababu timu ziliongezeka na kuzaa upinzani mkubwa na hata zilizokuwapo zilizidi kujiboresha na nyingi zilikua na wachezaji wa kigeni, kwahiyo ulikuwa msimu bora na upinzani," alisema Mynaco.

Kwa sasa wapo Watanzania watatu wanaocheza ligi hiyo kwa upande wa wanawake na hapa anaeleza wanapokutana.

"Tupo watatu mimi, Hasnath Ubamba na Suzana Adam, bato linakuwa kubwa sababu tunafahamiana lakini baada ya mechi undugu wetu unaendelea, tukiwa uwanjani kila mtu anapambania nembo ya timu yake."

Msimu huu Mynaco amemaliza na mabao manne na asisti nne kwenye mechi 28.